Msaada wanajamvi: Kuna hatari nikifanya hivi?

Msaada wanajamvi: Kuna hatari nikifanya hivi?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
34,181
Reaction score
99,193
Habari wakuu.
Tarehe 29 October, UTUMISHI waliita watu kazini, nikaitwa na mimi. Baada ya kupata barua toka kwao, nikaenda kituo cha kazi. Huko tukapewa form 3 za kujaza. 1. Personal details. 2.Next of Kin na 3.Medical Examinations. Nikapiga copy ya academic certificates nikaacha pamoja na passport size 3.
Hawakunipa barua ya ajira na wala siku sign mkataba wa kazi... Nikaomba ruhusa ya wiki 2 nije home kujipanga.
.
.
Leo tena UTUMISHI wakaita kazini, na mimi nipo tena. Naipenda zaidi hii nafasi ya saizi. Sio kwamba ile ya mwanzo mbaya, NO, zote sawa Tutor II, ila hii ya pili ndio direct na field yangu.
.
Je, kuna hatari yoyote kuwakacha wale jamaa wa mwanzo na kwenda kwa hii nafasi za pili?
 
mkuu kwanii usiende sehemu ya kwanza kumbuka wahenga walisema mchagua nazi huishia koloma fikiria mara mbili kwa hilo usije ukaingia kwenye mkenge kuna kitu cha lawson software utumishi wakikuingiza na ukipata chek no ya salary ukiacha ikiwa hivyo utaanza upya mtaani
 
thanks kaka. ila sija sign nao mkataba? yaani nilienda kuruport tu.
 
hapo haina shida mkuu,km hujaingizwa kwenye payroll we nenda kawe tutor tu ila km umeingizwa inabidi tu uendelee kuwa afisa mtendaji wa kata ,wale kupeleka details zako mpka wewe umalize ruhusa yako so usiporudi kule watajua umeingia mitini so hawatapeleka details zako kule hazina,hyo ningekuwa mimi ilikuwa nafasi nzuri sana ya kuchagua ninapotaka kufanya kazi.
 
mkuu KAKA YAKO NAPITA shukrani kwa kunipa moyo. wasiwasi wangu ni huo tu kwamba zile details nilizojaza kule kwa mara ya kwanza, si watakua wameshani blacklist UTUMISHI? kama alivyosema mkuu stranger man hapo juu?
 
Last edited by a moderator:
Una hatari maana ya kujaza zile fomu na kuacha copy ya vyeti ndio inayosaidia kutengeneza barua ya ajira na kuingizwa kwenye Lawson haimanishi kama hukusaini mkataba katika barua ya ajira itazuia wewe kuingizwa katika mfumo kama bado hujaingizwa kwenye mfumo unaweza kwenda kuripoti hyo sehemu nyingine but Fanya mawasiliano na Afisa Utumishi mueleze dukuduku lako wengine ni waelewa kama bado haingiza kwenye Lawson haina tatizo but kama tayari usipoteze muda rudi tu kituo cha awali.
 
Ndugu yangu...... Fanya kazi unayoipenda ili uwe na furaha na kaz yako

inaonekana uko interested na kazi hii ya pili

hata kama ingekuwa umesaini mktaba binafsi ningeendelea kukushauri kufanya kaz hii ya oili uliyodai ipo ktk field yako
 
mkuu haina shida mana bado hujasaini mkataba, ili uweze kuingizwa kwenye payroll lazima uwe umesaini mkataba pamoja na kujaza form zingine za ajira. But to be on a safe side, nenda kwa hr wa kituo cha kwanza umuelezee kwamba umechaguliwa sehemu nyingine na kwamba hutaenda huko.
 
shukrani wakuu. nitafanyia kazi mawazo. nitaanza na kwenda ofisi za kule kwa kwanza hafu niongee na hr. kama sijaingizwa kwenye system nitaenda station B.
 
Back
Top Bottom