Msaada wana JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wana JF

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by stephot, Jul 18, 2012.

 1. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,001
  Likes Received: 2,617
  Trophy Points: 280
  Msaada wenu wana JF,nina ndugu yangu amekamatwa Ijumaa 13/07/12 kosa ni kuwa ameokota simu ndani ya basi ambamo yeye hulala humo baada ya kazi saa 6 usiku,akampa mkewe mida ya mchana,mkewe alipoanza kuitumia ikatambulika kwenye mtandao,mchana siku iliofuata mkewe akakamatwa hatimaye mumewe na dereva wake wakakamatwa on same day,mke akatolewa kwa dhamana siku ya j.tatu 16/07/12,mume akabaki kwa kigezo cha kusubiri upelelezi ukamilike,walioibiwa simu wamearifiwa tokea j.tatu 16/07/12 ili waje kuwatambua wahusika mpaka leo hawajatokea,tumeomba jamaa yetu naye aachiliwe kwa dhamana tunaambiwa haiwezekani kwani kesi ni ya unyang'anyi na hiyo simu iliibwa kwa nyumba kuvunjwa,maelezo ni kuwa wakati jamaa yetu na dereva wake wakiwa wamelala kwenye gari usiku wa kuamkia tarehe 14/07/12 mida ya saa 9 usiku kuna mtu aliomba kulala kwenye basi lao na ilipofika asubuhi mida ya saa 11 alfajiri yule mtu aliondoka hivyo wazo ni kuwa ni yeye ndiye aliyedondosha hiyo simu humo ndani na dereva anasema anamfahamu kuwa ni dereva wa Day Worker hapo kituoni ila hajatolewa ndani ili kwenda kumtambua mpaka leo hii,sasa msaada ninao omba,nifuate utaratibu gani ili niweze kumtoa jamaa yangu au ni mpaka hao watu wanosadikiwa kuvunja nyumba na kuiba simu watakapopatikana?na je kama hao walioibiwa wakija kuwatambua na ikaonekana jamaa yangu hajahusika utaratibu wa kumtoa ni upi?pia kuendelea kukaa kwenye selo ya Polisi kwa muda wote huu ni sahihi?
   
Loading...