Msaada wana jamvi, mgongo unaniuma

johf1981

Member
Dec 13, 2016
13
3
Ndugu zangu,

Kuna tatizo mimi limenipata juzi, wakati najaribu kuinua mzigo dukani hivi kutoka chini kama wa kilo 15 hivi, nikasikia kitu mgongoni kama kimechoma hivi, basi tangu hapo mgongo unauma balaa hasa nikisimama wima kutoka kuinama, au nikiinama au kuchuchumaa. Wakati mwingine nashindwa kuinua kitu hata kama ni kidogo, yani najisikia kutamani kulala tu hasa kulalia mgongo.

Hii tatizo itakuwa ni nini, je litatibika na kuwa kama nilivyokuwa mwanzo? Nakosa raha sana na nashindwa kufanya kazi zangu za kila siku.


Tafadhali naomba nisaidieni
 
pole sana mkuu,ukipata suluhisho niambie na mimi nina jamaa yangu nae ana hilo tatizo akti anafanya kazi ya kuuza mazao alipokuwa akinyenyua mzigo alipatwa na hicho kitu kina msumbua sana
 
Mkuu hapo itakuwa pingili za mgongo kuna sehemu zimepishana!
Wahi hospitali iliyo karibu nawe then watakuandikia rufaa uende hospitali kuu mhimbili pale utakutana na madaktari bingwa wakuanzishia matibabu yapasayo.

Siku nyingine jitahidi kutumia mara kwa mara juisi ya maboga, bamia na mlenda hii husaidia kuweka uwiano wa kiwango cha utelezi katika joints za mwili wako wote hasa kama shughuli zako zinakulazimu kuinama na kuinuka mara kwa mara.
Zile clanes za pale bandarini haziwezo kuoparate bila kuwekewa girisi.

NB kipindi unasikilizia matibabu, punguza maumivu kwa kujichua na mchanganyiko wa tangawizi na mizizi ya ndulele/tulatula.
Get well soon...
Pole sana!
 
Jamani nashukuru sana kwa ushauri mzuri,bas ntajitahid kwenda hospital haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaid
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom