tata mvoni
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 534
- 81
Habari wakuu mwezi uliopita nilikuwa mjini MOROGORO nikifanya RESEARCH MOJA HIVI KUHUSU HALI YA UPATAIKANAJI WA MAJI KATIKA MKOA HUO sasa katika pita pita zangu nikawa nimeifikia nyumba moja iko mtaa wa BOMA ROAD kata ya huu ni mtaa ambao uko kamdoni mwa barabara iendayo ofisi za mkuu wa mkoa wa MOROGORO na uko katika kata ya MJI MKUU.Basi nikamkuta mama mmoja ila kwa mie ni sawa na bibi yangu tena anamzidi hata bibi yangu kwa umri. Huyu bibi anasikitisha kwa kweli kwanza kafiwa na mme wake pili alipatwa na kiharusi na kwa sasa ana kifaa anachotumia kwa ajili ya kumwezesha kutembea na kufanyia mazoezi tatu ana familia ambayo inamtegemea!!! Niliongea na huyu bibi mambo mengi ila lililonisikitisha ni kwamba kuna kijana wake amemdhulumu (sijui kama nimepatia) kiwanja na kumpa mtu mmoja hivi kutoka DAR ES SALAAM ambaye amejenga fremu za maduka kwa mkataba wa kumlipa kila baada ya muda fulani!! KIUKWELI BIBI huyu alinisumulia kisa hiki huku akilia!!! Nilimuonea huruma sana ila sikuwa na cha kumsaidia ila NILICHOAMUA NI KUWEKA HAPA JF ili watu wa gender waone jinsi ya kumsaidia huyu bibi ili apate haki yake.KAMA KUNA WA KUWEZA KUMSAIDIA ANAWEZA KUWASILIANA NAMI ILI NIMPE NAMBA YA NYUMBA NA JINA LA HUYO MAMA.