News Alert: Msaada wakisheria unahitajika

Mudugu

Senior Member
Mar 17, 2018
140
130
Napenda kuuliza hii ikoje
Nina kesi mahakamani ambayo nimeikatia rufaa kutoka mahakama ya wilaya kwenda mahakama kuu niliwasilisha rufaa yangu mwezi 10/2017
Nikapangiwa tarehe yakuludi mwezi 11/2017
Tarehe ilipofika tulienda nilitegemea nitapewa majibu ya pingamizi ya rufaa yangu lakini skupewa kesi ilipigwa tarehe mpaka mwezi 02/2018 tarehe ilipo fika tulienda ndo nikapewa majibu ya pingamizi ikionyesha tarehe iliyo jibiwa ni mwezi wa 11/2017 lakini mrufaniwa hayo majibu alinipa mwezi wa 02/2018 naona huo nikama ujanja wakutaka kunipiga chini ionekane kuwa nimechelewa kujibu kumbe yeye ndo aliye chelewa au hapo ikoje msaada wenu wanasheria nifanyaje hapo kesi ilipigwa tarehe mpaka mwezi wa 06/2018 nisaidieni asanteni sana
 
Kiongozi Mudugu cha kufanya ni kusubiri tu tarehe tajwa ya kesi (mwezi wa sita).
Kwa kawaida majibu ya rufaa hutakiwa kuwasilishwa mahakamani kwa ajili ya kusajiliwa (filing) ndani ya wiki mbili (siku 14) toka mujibu rufaa (mrufaniwa) apokee wito na nakala ya sababu za rufaa. Mujibu rufaa alipaswa kujibu ndani ya huo mda, vinginevyo majibu yake yanakuwa batili kama ruhusa ya mahakama haikutolewa kujibu nje ya mda.

Kwa upande wako ni kwamba inawezekana rufaa ilijibiwa ndani ya mda. tatizo lililojitokeza ni wewe kutopewa majibu hayo. Pia majibu yako ya kumjibu mrufaniwa si lazima katika mfumo wetu wa mwenendo wa mashitaka. Mwenendo wa kesi unamtaka mrufaniwa kujibu sababu za rufaa, na hailazimishi au haitoi ulazima wa mwomba rufaa kupeleka majibu yake akimjibu mrufaniwa. Hivyo wewe usihofu kwa hilo. Hata hivyo mahakama inayo mamlaka ya kukutaka kujibu hoja za mrufaniwa, lakini hiyo ni lazima kusubiri mpaka mahakama itoe maelekezo ya namna hiyo.

Kwa maneno mengine subiri tu siku tajwa uhudhurie mahakamani, na pasi shaka mahakama itatoa mwongozo wa kuanza kusikilizwa kwa rufaa yako.
Karibu
 
Asante sana ndugu Dragoon
Kwa kunipa mwanga na kunitoa wasiwasi
Ubalikiwe sana kiongozi
 
Back
Top Bottom