8.Fungua huduma ya water supply, Nenda idara ya maji jisajili na ulipie wakuvutie bomba.
Ukiwa nyumbani, Uza maji kindoo kidogo (lita 10) ni sh 50 na ndoo kubwa [ya lita 20] ni sh 100 kule Lake Zone sijui bei ya Dar.
Chongesha toroli 5 kodisha toroli 4 kila moja kwa siku ni sh 1000.
Halafu toroli 1 ilobakia ni yako usiikodishe, Nenda nyumba kwa nyumba uwaombe uwe unawasambazia maji kwa toroli wanakulipa au weka kijana kama unaona soo.
NOTE: Bei ya kutengeneza toroli moja kwa nondo na bomba ni sh 70K, Kwa matano ni 5X70K=350K gharama ya kuchomelea matoroli matano.
Gharama ya kuvuta bomba la maji kule Lake Zone kama haijapanda ni sh 150K ila hapo haujaweka vifaa vingine unaweza kuazima. Baadhi ya vifaa ni kama pipe wrench, tape, praizi/katapraizi, koki, mpira, connector, ulaji wa fundi, n.k.