Ondoa wasiwasi mkuu. Hiyo ni kawaida.
Kikawaida mtoto aliyezaliwa hupungua uzito kwa takribani 10% ya ule uzito aliozaliwa nao. Hii inatokea katika ile wiki ya kwanza (siku 7) kwa sababu mtoto akizaliwa anakuwa na maji mengi, hivyo kupungua kwake uzito inasababishwa na kupungua kwa hayo maji mwilini.
Kisha anaanza kuurudisha uzito alioupoteza ndani ya wiki 2 au 3 baadae, kwa kuwa atakuwa akiongezeka 15g-20g kwa siku.
Kwa hesabu rahisi tu, mtoto wako kama alizaliwa na 3.3kg, wiki yake ya kwanza alipoteza 10% ya uzito wake (0.33kg- kiasi alichopoteza), hivyo akabakiwa na kilo 2.9kg. Kisha akaanza kugain weight kwa 15g-20g per day kwa wiki 5 zilizobaki (siku 35) akaongezeka 0.5kg.
Kwahiyo tunategemea baada ya wiki 6 uzito wake uwe: 2.9kg+0.5kg= 3.4kg
Hizo ni estimation tu, sio lazima iwe exactly that weight.