Elfu arobaini (40,000) ilivyobadilisha maisha yangu na changamoto nilizopitia katika biashara

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
636
1,017
Wakuu poleni kwa majukumu ...

Nilimaliza kidato cha Nne 2013 na kujiunga na kidato cha tano 2014 na kuhitimu 2016 baada ya kuhitimu nilitoka mkoani Kilimanjaro na kuingia katika jiji la Dar es Salaam kuishi nyumbani kwa mjomba , wakati ulipofika wa kuapply chuo basi nilijikuta nafanya maamuzi ambayo wengi walinishangaa , nilichagua kusoma Open university of Tanzania ( OUT)
na nilifanikiwa kuchaguliwa kusoma hapo , nikiwa sina mkopo ukizingatia wanafunzi wengi mwaka ule wa kwanza wa Magufuli walikosa mkopo ,

Basi kutokana na msoto wa kuomba nauli na gharama binafsi nilijikuta nikiwaza kujiingiza kwenye biashara

Na biashara niliyoifikiria zaidi ilikuwa ni saloon ya kiume kwani nilikuwa tayari najua kunyoa , ila bado shida ikawa mtaji na eneo la kufanyia. Nilibana matumizi sana mpaka nikapata sh. 40,000 ambayo moja kwa moja niliingia Kariakoo na kununua mashine moja ya kunyolea kwa 35,000 na elfu tano nikanunua spiriti na kitambaa cha kumfunika mteja

Niliporudi nyumbani kwa uncle nilipokuwa naishi maeneo ya Mbezi Msakuzi barabara ya kuelekea Mpiji Magoe , basi nikawa nimewaza kurekebisha banda bovu la mbao lililokuwa karibu na barabara nyumbani kwa uncle na kubandika magazeti pembeni ili kidogo kupendeze na rasmi nikaanza kunyoa bila hata kioo wala kiti cha saloon.

Nilipata wateja kiasi kutokana na saloon nyingine kuwa mbali sana.

Nilitumia kama miezi miwili kupata tsh 170,000 nikaweka mkaa kwa kutumia 130,000 na 40,000 nikaweka pumba za mahindi , nikawa nauza hata nikiwa nimeenda chuo waliokuwepo nyumbani akiwemo pia dada wa kazi walinisaidia kuuza

Wakati wote huu nilikuwa natiwa moyo sana na uncle wangu , japo kabla ya kuanza chochote niliwahi kumuuliza , hivi nasoma namaliza halafu nakosa kazi maisha yangu yatakuwaje ?

Natamani kuingia kwenye biashara , alichonijibu ni kwamba nisome nikimaliza ataniajiri nikifikiria hakuna mfanyakazi wake anayelipwa hata laki na hamsini. Kauli hiyo ilinipa nguvu sana ya kutafuta njia mwenyewe ya kupita ndipo nikaanza saloon, mkaa, pumba na nikaelekea kuanza taratibu duka la mahitaji ya nyumbani nalo likakuwa vizuri sana, kimasihara tu japo nilianza kwa kuunga unga sana

Mwaka 2018 mwishoni nikapitia shida sana iliyonifanya nitoke kwa uncle niondoke na duka kwani fremu niliyokuwa natumia nayo ilikuwa ni contena lililotengenezwa vizuri kwa duka nyumbani kwa uncle, nilipitia mtikisiko mkali kwani sikuweza tena kuendelea na saloon , mkaa na pumba, nikajikita tu kwenye duka la mahitaji ya nyumbani , nikafanya vizuri tu nikanunua kiwanja nikashirikiana na kaka yangu kufungua duka la furniture handeni Tanga na mwaka 2020 basi nikafungua duka jingine na kuweka mfanyakazi

Mpaka 2021 mwaka jana mwezi wa kwanza duka moja lilipokumbwa na ukosefu wa wateja kutokana na sheria za eneo hilo za ulinzi shirikishi za kupangiana kulinda usiku wapangaji wengi wakakimbia na ndio walikuwa wateja wakuu

Nikalazimika kuhamisha biashara lakini ni kama mkosi nilipohamishia haukupita mwezi bomoa ikapita nikalazimika kuhamisha kwa kukurupuka hali ikawa mbaya sana nikalazimika kumaliza vitu nibadilishe biashara na fremu nyingine nilikuwa nimeshaiona na kuongea na mwenye fremu kuhusu plan niliyokuwa nayo na nitakuja kulipia kama baada ya wiki.

Ile nimemaliza kuliua duka bidhaa nyingine nikichanganya kwenye duka la pili ile kwenda kulipia nakuta mtu kacopy idea yangu kafungua kuuliza nani kafungua , nikaambiwa ni mwenye fremu kaingia mkopo kafungua, nilipaniki nikafanya kitu cha kijinga kutaka kwenda kujenga nikanunua tofali za kutosha kokoto na mchanga ile naanza tu ujenzi kukaibuka mgogoro wa ardhi niliyonunua mpaka sasa unaendelea ,

Sasa mpaka hapo ukizingatia nina ari kubwa kwenye utafutaji nilipanic sana hela niliyonayo ikaanza kuteketea maana haijizalishi nikaishia kufanya kosa lingine tena kununua pikipiki ambayo hata mwezi haukupita dereva niliyempa akapata nayo ajali ikawa skrepa , nilipaniki kuliko kawaida nikawa naogopa sana , basi ili kulinda duka la pili nikaingia mkataba na mfanyakazi asinipe hela yoyote kwenye duka hata iweje tuka-sign akiwa na mdogo wangu ili kulinda anguko langu lisihamie huko basi

Mimi nikawa nipo tu sina kazi ya kufanya , haikupita muda naye kaka akaharibu duka handeni na kufunga ,

Nilizidi kuwa mtu wa mawazo nakaa ndani tu , nikiwaza maisha yangu na nikifilisika itakuwaje nitadharaulika kiasi gani , ilikuwa wakati mgumu sana kwangu, basi nikawa najaribu kuomba kazi yoyote haswa mikoani nisikofahamika nikaishi huko tu ili kuzuia kabisa anguko la duka la pili na nisilitegemee kwa chochote faida yake ikuze zaidi duka na kutumika tu kunirudisha kiuchumi

Sikufanikiwa kupata kazi nikaamua kusafiri kwenda Mbeya bila hata kujua kuwa naenda kufanya nini , hela ya kuhama ni baada ya kuuza tv, redio , sofa na friji

Basi nikatua Mbeya nikapanga chumba na kuweka vitu vyangu kwani kitanda pia nilisafirisha,

Sikupata kazi yoyote na kukaa mwenyewe ni kama nilikuwa nazidi kupata msongo wa mawazo basi , nikawa nimeongea na jamaa mmoja Facebook yupo Iringa nikaenda kufanya kazi kwenye mashamba ya nyanya nikilipwa laki kwa mwezi , bila kumwelezea maisha yangu .

Iringa kazi ilikuwa ngumu sana chakula ni ugali na dagaa grade 3 wachungu hatari. kila siku asubuhi mchana na jioni. Wasukuma tu ndio walikuwa wanafurahia . Kulala kwenyewe kuwa tunalala chumba kimoja watu nane , hii sehemu niliitumia kama kujifunza kuishi kawaida hata kama hela ninazo na elimu. Pia ili nisaidia kuondoa msongo wa mawazo kwani shambani tulikuwa zaidi ya 17 kwahiyo muda wote ulikuwa makelele na utani mwingi . Hata bosi hakunijua maisha yangu mara nyingi alijisifu kufika form six mbele yetu .

Wafanyakazi wote waliishia darasa la saba isipokuwa mimi ambaye nilificha ukweli wangu wote japo wote walikuwa wananiheshimu sana bila kunijua .

Baada ya kutoka huko Iringa nilirudi nyumbani Moshi kwa harusi ya kaka yangu na baada ya kutoka huko basi nilirudi Dar na kuelekea Mbeya ambako nimefanikiwa kufungua bar ,
Na ndio nipo huko nikipambana nirudishe na lile duka tena na kuwa na maendeleo mazuri ninayo yatamani .

Niwashukuru wote,
 
Samahani Sana ndefu kusoma Nina mifumo mingine naendelea nayo
JPEG_20220707_173505_1263858611972680651.jpg
 
Wakuu poleni kwa majukumu ...
Nilimaliza kidato cha Nne 2013 na kujiunga na kidato cha tano 2014 na kuhitimu 2016 baada ya kuhitimu nilitoka mkoani Kilimanjaro na kuingia katika jiji la dar es salaam kuishi nyumbani kwa mjomba , wakati ulipofika wa kuapply chuo basi
Makini Sana mkuu
 
Wakuu poleni kwa majukumu ...
Nilimaliza kidato cha Nne 2013 na kujiunga na kidato cha tano 2014 na kuhitimu 2016 baada ya kuhitimu nilitoka mkoani Kilimanjaro na kuingia katika jiji la dar es salaam kuishi nyumbani kwa mjomba , wakati ulipofika wa kuapply chuo basi
Hivi nyie watu wa Moshi mnangaika na kuteseke hivyo unafikiri mlitumwa pesa kwenu loh!! mimi niangaike kwenye shamba la nyanya mshahara 100k, life is not all about money, life is beyond money
 
Congratulations kwa fight ya namna hii at your age. Tulio wengi umri huu na kisomo ni patashika. Mshukuru Mungu kukupa upeo mapema. Kukua kwa mwanaume na pamoja na uzani wa upeo. Kudos nyingi Braza
 
Maisha ni safari ndefu, kupanda na kushuka kupo...

Tunafanana ki historia pakubwa.. Nilikutangulia kumaliza shule, nilianza harakati mapema, nilitoboa mapema, kkisha maseke yakatokea, sijarudi kwenye mstari mpaka leo hii, nachechemea kimtindo, nipo sehemu nashukuru Mungu (nisikufuru) ila si pale ambapo ndoto zangu zilikuwa.
 
Nazitafuta nikifika miaka 30 now bado 4 ya kufight niishi kwa raha
Inaweza kua tofauti ndugu, mimi nikiwa na miaka 24 nilikua napambana mno kwa siku si chini ya saa 14 mpaka 16, jamaa mmoja akaniambia nikifika miaka 30 nitakua mbali sana kimaisha. Badala yake sasa ingawa siko vibaya sana lakini niko 35 hali bado sio njema.
 
Inaweza kua tofauti ndugu, mimi nikiwa na miaka 24 nilikua napambana mno kwa siku si chini ya saa 14 mpaka 16, jamaa mmoja akaniambia nikifika miaka 30 nitakua mbali sana kimaisha. Badala yake sasa ingawa siko vibaya sana lakini niko 35 hali bado sio njema.
Usikate tamaa, pambana, siri ya mafanikio
"struggle , struggle and struggle with God in your Struggle"
 
Maisha ni safari ndefu, kupanda na kushuka kupo...

Tunafanana ki historia pakubwa.. Nilikutangulia kumaliza shule, nilianza harakati mapema, nilitoboa mapema, kkisha maseke yakatokea, sijarudi kwenye mstari mpaka leo hii, nachechemea kimtindo, nipo sehemu nashukuru Mungu (nisikufuru) ila si pale ambapo ndoto zangu zilikuwa.
Jitathmini usije ukawa bado unakula bata zile zile matumizi bado ni kama yale ukiwa juu, maana hiyo ndio inafanya wengi wanashindwa kupanda tena , kwa kipato kuishia kwenye matumizi na kukupoteza zaidi jitathmini
 
Congratulations kwa fight ya namna hii at your age. Tulio wengi umri huu na kisomo ni patashika. Mshukuru Mungu kukupa upeo mapema. Kukua kwa mwanaume na pamoja na uzani wa upeo. Kudos nyingi Braza
Shukrani
 
Back
Top Bottom