Msaada wa ushauri kuhusu solar Power

Msaada wa ushauri kuhusu solar Power

Je umefunga charge control au bado? Labda nikukumbushe kuwa sora raha yake ni nilizevu ya moto. Ukitaka ufaidi sora hata kwa panel kama hiyo funga betri kubwa ya N 150 _ 200. Halafu usitumie betri mpaka ijae kama una charge control Kama huna charge control utaua betri mara moja na pia hiyo betri yako ni ndogo sana itatumika kwa muda mfupi sana .Kumbuka taa kutumia DC badala ya AC na taa zichukulie kwenye charge control ili usiwe unakomba kabisa moto.
Ahsante kwa ushauri wako. Charger Control ninayo, ila naona betri ni ndogo km ulivyoshauri na nahisi imeshakufa mana nikiweka maji haifanyi kazi(haisukumi moto).
 
Unaweza kufanya hivyo vizuri sana na tena unaweka automatic switch kutoka TANESCO kwenda solar au hata generator. Vifaa hivyo vipo madukani nenda Kariakoo. Ukitaka kuinjoi solar fanya isiwe ndogo sana iwe kuanzia 200 watts hivi, mimi nafanya mambo mengi sana na 200 watts tv, laptop kuanzia asubuhi hadi saa 11 jioni na tena masaa 2 tv kuanzia saa 2 hadi 4 na tena taa 5 zinabaki zikiwaka nje hadi asubuhi. Hapo mchana natumia blenda, pasi, nk. Ukiwa na pesa solar ni safi saana!
Shukrani kaka..
 
Unafanya uamuzi mzuri sana wa kuwa na solar power. Navyo andika hapa mimi nipo mbali kijijini Morogoro hakuna umeme wa Tanesco lakini naatumia laptop kuanzia asubuhi hadi jioni ipo kazini, Tv kubwa ya tumbo ipo on mda mrefu tu wa mchana na usiku naangalia walu masaa 2. Taa 5 each 5watts zinawaka nje usiku kucha achilia mbali zile za ndani. Natumia blenda ya juice, pasi ya solar, nachaji simu, nk. Hayo yote ni kwa panel 2 zenye kutoa watts 200 kwa jumla. Nina inverter ya watts 600 na charger ya amps 20. Nina battery moja tu ya maji Amph 100. Sijawahi kujuta au kukosa umeme tangu niweke solar hii mwaka 1 uliopita. Kama unataka kuwa na friji na feni napendekeza uifanye iwe na uwezo mara 2 hivi ya hii ya kwangu.

Nunua panels za watts 400, solar charger amps 30, inverter watts 1000 na battery 3 kila moja Amph 100. Hii system utaweza kupampu maji kutoka kwenye kisima pia na kweli utakuwa huru na Tanesco.

Usinunu battery zile wanaita dry battery kwani sio nzuri kama za maji (uzoefu wangu). Utakapoweka panel zako ziwe pasipo na kivuli na mwelekeo wake kama ni juu ya bati basi ziwekwe on flat surface, kama unaweza jenga mnara mfupi ardhini weka panel juu yake inategemea na usalama uliopo, fanya mnara huo uwe rotatable yaani unaweza kuuzungusha kufuata mwelekeo wa jua na hapo utaongeza ufanishi ya system yako kwa 30%. Enyoy.


hivi hizi hesabu mmesomea wapi ?? mbona unabuni buni mkuu ...yani watts 400 afu unataka uwe na betri tatu za 100Ah really ?? hujui kuwa solar ya uwezo huo inaweza toa 23Ah tu kwa masaa nane kwa siku ni 188Ah sasa hizo nyingne unajaza na nini
 
NINA SOLAR PANEL WATT40 BETRI n33

NILIKUWA NAITAJI INVETA LAKINI WATU WAKANISHAURI KWAMBA NIKITUMIA
MOTO UTAKUWA UNAKATA MAPEMA

NA MIMI NATAKA NITUMIE TV

NIMEKUJA KWENU WATAALAMU NAOMBENI MSAADA PLZ
 
Back
Top Bottom