Msaada wa ushauri katika hili; Blind decision

doleicute

Member
Oct 18, 2017
76
42
19/02/2009 saa sita usiku baba wa mtoto wangu (hatukuwa tunaishi pamoja) alinieleza kwa simu kuwa hanihitaji tena na ile barua ya posa alotoa tuisahau na maelezo juu ya malezi ya mwanetu akasema yeye anao watoto wengi so huyu mmoja hana shida nae

NAMNUKUU
: "Nina watoto watano huyo mmoja nakushauri katafute mwanaume yeyote asiye na uhakika wa kizazi chake mpe kama zawadi". hapo binti yetu alikua na umri wa mwaka mmoja na miezi mitano. After that phone call hakuonekana tena mpk baada ya miaka miwili aliporudi na kuomba radhi kwamba mambo yake hayaendi sawa na anahisi labda nimemuwekea kinyongo ndio maana anazidi kushuka kimaisha.

I told him the truth that yes niko na maumivu because of ugumu wa maisha and yet im still lonely with no other income but mimi sio nliokufungia riziki and if your apologies comes from your heart then go with Peace ila kama ni dhihaka na majaribio kwa mungu you will find a lot of problems in your plate.

Aliondoka na hakugeuka nyuma, i suffered alot enough to poison myself with any kind of harms. nliamua kufanyakazi za ulinzi na kufanikiwa kupata lindo moja zuri ktk kampuni moja hapa dsm.

Japokuwa ilinibidi kupitia mapito mengi magumu ili kukidhi mahitaji ya mwanetu ikiwemo shule, pango,kula na matibabu (baba yake ni manager máhusiano ttcl) nlilala na wanaume tofauti ili kupata mahitaji ya binti yetu (nashukuru mungu alinilinda na maradhi).

Ndugu zake na baba yake waliingilia kati hili jambo lkn kwakuwa walimtegemea sana ndugu Yao kimaisha(maana ndiye aliyekuwa na uwezo) ilibidi washindwe kumkosoa deeply kwa hili so namimi nlikata tamaa kupata msaada wowote kutoka kwao.

After almost seven years since he abonden us huku nkiwa ktk hiyo kampuni ya ulinzi(nlikua nkisoma pia na kufanikiwa kupata diploma) nkabahatika kupata ajira ktk international organization(Diplomatic mission) hivi sasa npo kzn kwa miezi nane na binti yetu yupo Diamond primary school sasa (drs la tatu) yule mzazi mwenzangu kumbe alikumbwa na kashfa ya kukopa hela ktk mabenki mengi pamoja na mikopo binafsi ya riba na kushindwa kulipa sasa amesimamishwa kazi na wanataka kutumia mafao yake kulipa madeni hayo huku wadai wengine wakitangaza mali zake alizoweka rehani kuuzwa minadani kama fidia ya madeni Yao (kwakweli hili linaniuma hasa coz ana watoto).

Amesikia kuwa nina kazi nzuri na binti sasa anaishi nakusoma vizuri than alivotuacha ktk kachumba kasiko na umeme wala sakafu. Amemtuma mshenga wetu eti anitafute na atukalishe chini coz amegundua kosa lake na yupo tayari kutubu maisha yaendelee.

Swali langu kwenu ndugu zangu.

1.Nikimchunia ntahukumiwa na binti yetu kweli maana all i care is about our daughter and not him.

2. Kwa mfano akiniomba hela nkampa je hawezi niloga huyu kweli (kutokana na roho yake aliyoionyesha kwanzaa)
 
Asante dear.. Moyoni sina upendo uliobaki juu yake waswas wangu ni juu ya mtoto
Unaweza ukamwambia mtoto ukweli, na ukamweka wazi kwa yote, nachokwambia tu, "Kama anakuomba hela ukipendezwa mpe lakini asije akakurubuni tena ukaja kuishi nae, kumbuka alivo kutenda, usilipize msaidie kwa utakavopenda lakini usimruhusu akawa karibu yako tena.
 
Asante Sana... Hivo busara ni ipi nimwite kwa wazee na kumuweka wazi kuhusu ukaribu nami au nmtimue huyo anaenisumbua kila mara nyumban (mshenga) au nihame
 
Ushauri wangu uko hivi:-

1) Never put temporary people in the permanent place of your life.

2) Never hesitate to remove the wrong people from right place of your life.

3) Be strong and bold in important decisions about your life and family.
Thank you kaka.. I got your point and I will work on it... Barikiwa
 
Akiomba hela mpe kama utakuwa nayo, akitaka kumuona mwanae mruhusu akikutaka ww hapo ishu nyengine tena nadhani maamuzi zaidi yatatoka kwako
 
Kwanza mwambie ukweli mshenga, kwamba amwambie umemsamehe kwa yote, ila asahau kuhusu kurudiana na wewe, asipo sikia mwite kwa wazee umwambie hayo mbele yao ila kama moyo wako unampenda japo ya kukufanyia hayo yote unaweza kumrudia ila ni hatari kwako.
 
Asante Sana.. Ushaur huu nitaufanyia kazi mapema Sana coz I'm tired na usumbufu wao kwasababu mara ya kwanza mshenga wake aliponipigia simu na kuhitaji kuniona nlimkaribisha nyumban so anapajua na wamekuwa very excited kujua ni wapi nafanyakazi lkn sikuwaonyesha.. Barikiwa kaka yangu
 
Nilipo maliza kisoma huu uzi, nikagundua kwamba bado unampenda sana huyo mzazi mwenzio.
Nihilo tu kwa leo
Hahhaaaa kumpenda kimapenzi no no noo sina hisia za kimapenzi kabisa juu yake... Hilo hapana hahhaaaa Asante ndugu yangu
 
Akiomba hela mpe kama utakuwa nayo, akitaka kumuona mwanae mruhusu akikutaka ww hapo ishu nyengine tena nadhani maamuzi zaidi yatatoka kwako
Asante kaka wangu... Awe na amani tu kuhusu mwanetu ila juu ya Moyo wangu kanifunga kumpenda yeyote yule najipenda mwenyewe tuuu
 
Asante Sana.. Ushaur huu nitaufanyia kazi mapema Sana coz I'm tired na usumbufu wao kwasababu mara ya kwanza mshenga wake aliponipigia simu na kuhitaji kuniona nlimkaribisha nyumban so anapajua na wamekuwa very excited kujua ni wapi nafanyakazi lkn sikuwaonyesha.. Barikiwa kaka yangu
Amen, nawe pia, kwenye ulinzi hapo umenigusa sana, moyo umeniuma ukizingatia wewe ni mwanamke na kazi hizo navozijua ni za hatari, Daah MUNGU azidi kukupigania na azidi kukufuta machozi kwa kukuzidishia mema.
 
Asante kaka wangu... Awe na amani tu kuhusu mwanetu ila juu ya Moyo wangu kanifunga kumpenda yeyote yule najipenda mwenyewe tuuu
Sio sahihi kwa sababu sio wanaume wote tupo hivyo so mmoja akiharibu isiwe sababu ya ww kutopenda tena huenda bado chaguo lako hujapata
 
Amen, nawe pia, kwenye ulinzi hapo umenigusa sana, moyo umeniuma ukizingatia wewe ni mwanamke na kazi hizo navozijua ni za hatari, Daah MUNGU azidi kukupigania na azidi kukufuta machozi kwa kukuzidishia mema.
Amen amen kaka.. Sikuwahi kukata tamaa hivyo nlisema kheri nife mimi mwanetu aishi nkasema ntafanya kazi yoyote iliyo halali.. Can you imagine 150,000 per month.. Lkn Alhamdulillah mungu hajanitupa japo ile Kaz ni ngumu jaman
 
Back
Top Bottom