Msaada wa ushauri: Je, asitishe kwanza upande wa mwanaume kumtolea mahari?

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
Ni mdada ana mchumba wake wana mwaka sasa

Jamaa amekua na tabia ya kuwasiliana kwa siri na wanawake na dada akigundua jamaa anaomba msamaha yanaisha. Jumamos wazazi wa mume wamepanga kuja kupanga mahari.

Sasa Jana wakati wanaongea bidada kagundua jamaa ana simu nyingine ambayo yeye haijui na anawasiliana na mwanamke mwingine. Kamuuliza jamaa amekataa kutoa namba za huyo Dada wala hata kuomba tu msamaha

Bidada anadai asitishe zoezi mpaka jamaa atakapoamua kuexplain juu ya hilo au kumuweka wazi bidada juu ya hiyo simu

Anaomba ushaur wenu
 
Ni mdada anamchumba wake wanamwaka sasa,,,,jamaa amekua na tabia ya kuwasiliana kwa siri na wanawake bdada akigundua jamaa anaomba msamaha yanaisha
Jmos wazazi wa mume wamepanga kuja kupanga mahari.
Sasa Jana wakati wanaongea bidada kagundua jamaa anasimu nyingine ambayo yeye haijui na anawasiliana na mwanamke mwingine
Kamuuliza jamaa amekataa kutoa namba za huyo Dada wala hata kuomba tu msamaha,,,,
Bidada anadai astishe zoezi mpaka jamaa atakapoamua kuexplain juu ya hilo au kumuweka wazi bidada juu ya hiyo cm
Anaomba ushaur wenu
Aiseee
 
1. Mtajie idadi ya wanawake duniani hususani kwa sensa ya 2017 compared to idadi ya wanaume.

2. Ajiasses kwanza mapungufu yake ambayo yanamfanya huyo mwananume awe hivyo kabla hajafanya maamuzi ya kijinga.

3. Ajaribu kujishusha na kuomba msamaha kwa jamaa endapo kuna kitu alikosea na hakukijua.

4. Ana haki ya kusitisha hiyo process endapo tu ni mcha MUNGU, kama ni wale wa tia maji tia maji hajijui hata uhusiano wake na MUNGU ukoje basi mwambie akomae tu na jamaa mpaka kieleweke. Mtu anayemjua MUNGU kwa undani hawezi kuwa hadi hapo hajui afanyeje na wala hawezi kufika kwenye hiyo situation.
 
Kwani kwake kipao mbele chake ni kuolewa?

Kama ndoa sio kipao mbele aendelee na malengo yake mengine

Kama ndoa kwake lazima avumilie yanayo mkuta
 
hii ni story ya bidadada na jamaa, wafamishe tu kwamba waendelee tuu na mipango yao
 
Km amemkamata na kosa na hakua tayar kukiri hapo hana chake ajiondoe mapema maana akisema anachotaka ni msamaha atapewa wa kulazimisha na si wa moyoni
kafata msimamo wa kiume huwa wanasema "mwanaume hakuna kukiri kosa wala kuomba msamaha" hata akidakwa live anagegeda aseme kuna kitu kadondosha ndani ya papuchi anakitafuta hakuna kukubali.
Hello men....nawasalimia
 
kafata msimamo wa kiume huwa wanasema "mwanaume hakuna kukiri kosa wala kuomba msamaha" hata akidakwa live anagegeda aseme kuna kitu kadondosha ndani ya papuchi anakitafuta hakuna kukubali.
Hello men....nawasalimia
Lkn eve kwa uchumba mbona ni hali ya hatari? bora ingekua ndoa
 
Yaani mwanaume kaamua kukutolea mahali unaleta shobo? Mkikaa hadi 40 bila kuolewa mnalalamika hamna bahati!! Kama anamtaka huyo wa kwenye Simu kwa nini ahangaike na wewe hadi kukutolea mahari!? Hebu mwite hapa tumchambe huyo shogako asiyejitambua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom