Msaada wa ujuzi na kuendeleza biashara yangu ya mazao

saidi yakoub

Member
Nov 1, 2015
21
22
Habari zenu,

Mimi ni kijana ambaye nimemaliza kidato cha nne mwaka 2007. Nilibahatika kupata div 4 ya point 26 nilipata C tatu.

Sikubahatika kuendelea advance nikaamua kujishughulisha na biashara ndogondogo, huwa nafanya biashara ya mazao na huwa napata mpaka milioni 20 kwa mwaka, tatizo langu ni kwamba sina ujuzi wa kuiendeleza biashara yangu na mimi nataka biashara inayoendana na wakati.

Je nifanye nini ili niendeleze biashara yangu na jee kwa elimu yangu nisomee kitu gani ili niwe mjuzi wa biashara isinipige chenga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hongera sana kwa kufanya maamuzi sahihi na kutopoteza muda huko mashuleni, kuhusu elimu gani upate me nadhani experience uliyonayo ni elimu tosha kabisa. Nachotaka nikwambie kuhusu biashara ya kisasa, kwako nadhani unachotakiwa ni kukuza biashara yako tu ili faida iwe inaongezeka kila mwaka means capital lazima ikue. Nina swali hapa huwa unasafirisha na kwenda kuuza kwa rejareja au huwa unanunua na kuweka store then bei ikipanda unauza? Pia napenda kujua unafanyia mkoa gani kazi zako? Asante
 
Huwa nanunua na kuweka stoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa nanunua na kuweka stoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana hiyo inalipa sana, japo hujataka kuniambia unafanyia wapi mitikasi zako, lakini nakushauri fanya mpango wa ku add value yani unaweza kigrade huo mchele na kupak then unasambasa kwa jumla jumla kwa wauzaji wa rejareja the same goes to mahindi unaweza kusaga na kupak super sembe. Cha muhimu zingatia ubora wa bidhaa zako. Ungesema upo mkoa gani ingekuwa rahisi kuongea mengi zaid. Piga kazi dogo.
 
hongera kaka kwa hilo...sasa cha msingi hakikisha wateja wako wanafurahia bidhaa zako..ni vizuri pia ukajumuika na watu wenye hayo maujanja ili utanue mawazo yako...experience ni muhimu hata kuliko masomo ya darasani ila elimu ya darasani pia ina nafasi yake
 
Achana na kusoma kwanza kwa kipindi hiki.... pili hakikisha unatanua biashara kwa kuzungusha pesa kwa mazao mengine tofauti tofauti... uaikubari kukaaa hata miezi miwili na pesa mkonon bila kuizungusha... my friend utakua unatwanga maji kwenye kinu... hakikisha una roster ya manunuzi...
Eg.

Mahind wa 6 had 7.
Maharage yanafata.
Korosho.
Kilimo.
...

Uo ni mfano wa mazao katika misimu inayofanana... yaaani faid ya mahindi inanunua maharage... faida ya maharage unanunua korosho... faida ya korosho... unaizungusha kwingine.......

Then uwe na mahesabu sahihi... usiache hata tsh mia katika mahesabu.. hadi nauli na vocha uandikie...

Sent from "La -Vista"
 
Habari zenu,

Mimi ni kijana ambaye nimemaliza kidato cha nne mwaka 2007. Nilibahatika kupata div 4 ya point 26 nilipata C tatu.

Sikubahatika kuendelea advance nikaamua kujishughulisha na biashara ndogondogo, huwa nafanya biashara ya mazao na huwa napata mpaka milioni 20 kwa mwaka, tatizo langu ni kwamba sina ujuzi wa kuiendeleza biashara yangu na mimi nataka biashara inayoendana na wakati.

Je nifanye nini ili niendeleze biashara yangu na jee kwa elimu yangu nisomee kitu gani ili niwe mjuzi wa biashara isinipige chenga?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mchele unao? Unauza bei ghani kwa gunia
 
Tafuta masoko nje ya hapo ulipo! Faida unayopata jitahidi kutenga fedha kdogo,tembea maeneo tofauti kujifunza wenzako wanafanyeje,na nakufanya research ,onana na walikutangulia kwenye haya maswala jishushe ata kama umewaZidi ......
 
Back
Top Bottom