Kendrick Rama
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 409
- 458
Habari zenu wakuu,
Naomba mwenye uelewa au mtaalamu wa mambo ya magonjwa ya macho anisaidie hili.
Hapo juzi kati niligundua kuna kauvimbe kadogo ndani ya macho yangu ambacho hakana maumivu yoyote, ila baada ya kuchunguza kwa umakini na kuulizia baadhi ya watu walinambia kuwa huyo ni mtoto wa jicho na ndio kwanza anaanza, wengi wamenielekeza dawa mbalimbali za asili ila hadi sasa hakuna niliyotumia kwani siwezi kujaribu kila dawa kwenye macho yangu kwani ni kiungo muhimu.
Naomba kama kuna mwenye uwezo wa kunisaidia haya:
- Kujua chanzo chake kikuu ni nini?
- Kujua kama hapa naweza kuwahi tiba na kama nikichelewa Madhara yake ni nini?
- Kujua kama kuna uwezekano wa kupona?
- Madhara yake kwa ujumla?