Msaada wa soko la kuku wa nyama

Pretty P

Senior Member
Dec 27, 2010
121
20
Habari zenu wapendwa?

Naombeni msaada, mimi ni mfugaji wa Kuku wa nyama namshukuru Mungu najitahidi na napata matokeo mazuri Kuku ni wakubwa wanaridhisha,

Tatizo langu ni kupata soko zuri/wateja Naombeni msaada wenu ktk mbinu au njia nzuri yakupata wateja nakum maintain uyo mteja nisimpoteze.

upload_2017-4-28_13-38-29.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inajulikana soko la kuku lipo dar.... tembelea kwenye mahotel na mashule binafsi....

Msimu wa sikuu za waislam unakaribia.... Kama upo dar piga piga misele
 
Always usianze production kabla ya kujuwa watumiaji wa bidhaa zako ni akina nani au utawapataje. Hapo sasa inabidi uanze kusaga soli kuwatafuta. Ukumbuke wafugaji wa hao kuku nao wapo wengi na tayari wapo na wateja wao. Ila isikate tamaa. Mwanzo huwa mgumu kwa kuwa tunaanza biashara kinyume nyume.
 
Always usianze production kabla ya kujuwa watumiaji wa bidhaa zako ni akina nani au utawapataje. Hapo sasa inabidi uanze kusaga soli kuwatafuta. Ukumbuke wafugaji wa hao kuku nao wapo wengi na tayari wapo na wateja wao. Ila isikate tamaa. Mwanzo huwa mgumu kwa kuwa tunaanza biashara kinyume nyume.
Okay ngoja niisage kweli wagaba nitafanikiwa
 
Habari zenu wapendwa?
Naombeni msaada, mimi ni mfugaji wa Kuku wa nyama namshukuru Mungu najitahidi na napata matokeo mazuri Kuku ni wakubwa wanaridhisha, Tatizo langu ni kupata soko zuri/wateja Naombeni msaada wenu ktk mbinu au njia nzuri yakupata wateja nakum maintain uyo mteja nisimpoteze.
c6a536e13d9669240bb8f9c8b8038fb6.jpg
 
Una idadi gani mkuu na unaingiza kwa awamu kabla hawajaisha au mpaka mfugo mmoja ndio unaingiza wengine.

Pia sio mbaya nikajua na bei yako pia.

Shukran.
Nina Kuku 300 Mpaka 400 Na hii ni bunch Moja Na naingiza kila week. Bei 6500tsh tuu ni wakubwa
e03e3eee4d5b10f1e7c1e2dabb79017a.jpg
 
Nina Kuku 300 Mpaka 400 Na hii ni bunch Moja Na naingiza kila week. Bei 6500tsh tuu ni wakubwa
e03e3eee4d5b10f1e7c1e2dabb79017a.jpg

Mkuu, ulishawahi kuuza au ndio mara yako ya kwanza kuuza kiongozi.

Hiyo bei ya 6,500 sina hakika kama wanachukua kwa bei hiyo ila nnavyojua ni 5,500 imezidi sana sidhani kama inafika 6,000 kwa mteja anayechukua kuku wengi idadi ya mia naa.

Kama ni 6,500 labda kama wanachukua kidogo kidogo kwa bei hiyo ni sawa. Au aidha uwe na tender sehemu unapeleka mwenyewe lakini sio kwa kumuuzia mtu halaf nae akauze nadhani haitamlipa.

Najua chakula kimepanda sana na kuku kwa sasa ni wa tabu kiasi ila kwa bei hiyo waweza uza kama nilivyoainisha hapo juu.

Hapa home tuna kuku 2,000 tunaingiza kwa batch pia ila jamaa huwa anakuja kuchukua let's say kuku 400 huwa anachukua kwa 5,500 you can see hata 6,000 haijafika. It depends.

Ila nisikukatishe tamaa mamii nnachojaribu kufanya ni kushare nilichonacho pamoja nawe. Ila jaribu kupata mteja kabla hawajafika muda wa kuuzwa coz wakifika hapo ikiwa bado hujapata mteja nadhani unajua kitakacho tokea mamii. Wataendelea kula by the time unapata mteja siku, utakuwa umelisha zaidi au hata kugusa faida au msingi.

Mark my words. Karibu.
 
I wish kila mfugaji angekuwa anafanya hesabu zake vizuri kabla ya kufuga,inasikitisha kuona mfugaji anafuga kwa mazoea ili mradi ifikie muda wa kuuza hata kama asipopata faida.kwa kifupi ni kwamba ukifuga kuku chini ya 600 hautakaa uione faida kamwe utaishia kusema ufugaji haulipi na ufugaji huo hautaweza kubadilisha maisha yako daima!bali utaishia kupata hela ya kuwalisha,kuwahudumia,na madawa tu.simaanishi kwamba usianze kufuga hata hao kidogo kama ndio uwezo wako but jaribu kuwa na malengo ya kufikisha idadi kubwa zaidi.
just know that break even quantity kwa kuku inaaanzia kwa idadi ya 600 vinginevyo ni kama unacheza mduara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom