Mkuu, ulishawahi kuuza au ndio mara yako ya kwanza kuuza kiongozi.
Hiyo bei ya 6,500 sina hakika kama wanachukua kwa bei hiyo ila nnavyojua ni 5,500 imezidi sana sidhani kama inafika 6,000 kwa mteja anayechukua kuku wengi idadi ya mia naa.
Kama ni 6,500 labda kama wanachukua kidogo kidogo kwa bei hiyo ni sawa. Au aidha uwe na tender sehemu unapeleka mwenyewe lakini sio kwa kumuuzia mtu halaf nae akauze nadhani haitamlipa.
Najua chakula kimepanda sana na kuku kwa sasa ni wa tabu kiasi ila kwa bei hiyo waweza uza kama nilivyoainisha hapo juu.
Hapa home tuna kuku 2,000 tunaingiza kwa batch pia ila jamaa huwa anakuja kuchukua let's say kuku 400 huwa anachukua kwa 5,500 you can see hata 6,000 haijafika. It depends.
Ila nisikukatishe tamaa mamii nnachojaribu kufanya ni kushare nilichonacho pamoja nawe. Ila jaribu kupata mteja kabla hawajafika muda wa kuuzwa coz wakifika hapo ikiwa bado hujapata mteja nadhani unajua kitakacho tokea mamii. Wataendelea kula by the time unapata mteja siku, utakuwa umelisha zaidi au hata kugusa faida au msingi.
Mark my words. Karibu.
Naomba nikutembelee ndugu