Mkuu kwanza ukifuta na gallery huwa hazifutiki video zote, kama member wa humu unatakiwa ujifunze kutumia file manager.
Nenda kwenye list ya application zako tafuta file manager inaweza kuitwa my files ama files mara nyingi huwa na picha ya folder.
Ingia kisha tafuta folder linaitwa whatsapp kisha whatsapp media kisha whatsapp video utaziona hapo video za whatsapp. Unaweza pia ku click sent utaona video ulizotuma na whatsapp, hazina maana zinajaza tu nafasi unaweza kuzifuta na hizi huwa hazionekani kwenye gallery kikawaida.
Alternative nenda playstore download gallery nyengine.