Msaada wa sheria ya mirathi

mbapa

Member
Feb 4, 2014
63
18
Habari ndugu wana
Jf?.
Naomba msaada wa kisheria kwa urithi wa watoto kwa baba aliefariki akiwa na watoto4 pamoja na mkewe!. Akaacha wosia kwamba watoto wawil kati ya hao hawatamrithi chochote mana hawakumtii kama baba na walikua majeuri. Watoto hao wawil walionyimwa urithi kwa baba wao ndio wakubwa katika familia ya huyo baba, yani mtot wa kwanz na wapil!. Na baba hakuacha wosia huo kwa ushahidi wa maandishi wala sahihi, badala yake alikua anatamka tu mbele ya familia nzima isipokua watoto wanaonyimwa urith hawapo hapo mana wameshatengana na baba kwa kutokuelewana na baba. Je, kisheria mahakama itagawaje urithi huo?.
 
Mkuu mbapa,tambua mambo yafuatayo. Mosi,wosia si lazima uwe wa maandishi. Wosia wa maneno waweza kubishaniwa na kuthibitishwa mahakamani. Mashahidi waweza kuwa waliosikia marehemu akitamka jambo hilo.

Pili,mahakama haigawi mali za marehemu. Mahakama humteua Msimamizi na kumsimamia katika kutekeleza majukumu yake kama Msimamizi.

Tatu,taratibu za kuteua Msimamizi wa Mirathi,za kimahakama,zapaswa kufuatwa. Hiyo itatoa nafasi ya kujibiwa kwa hoja zenye ubishani baina ya warithi.

Nne,uhalali wa wosia utategemea masharti yatakiwayo na dini ya marehemu au kabila lake. Yategemea aina ya maisha aliyoyaishi marehemu kama ni ya kidini au ya kimila/kikabila. Kila dini au kabila lina sifa za wosia unavyopasa kuwa.
 
Last edited by a moderator:

Hapo kipengere cha (pili)
Msimamizi alieteuliwa endapo ataenda kinyume katika kugawa mali, mfano kampa mototo wake nyumba ambaye hakustahili na Hakimu akapitisha shauri lile. Hatua gani zifuatwe kupinga?
 
Huwezi kumnyima urithi mtoto wako Bila sababu za msingi kama ilivyoainishwa kisheria. (CUSTOMARY DECLARATION ORDER 4) yahusika. Wafanye kama Mselewa alivyoshauri.
 
Hapo kipengere cha (pili)
Msimamizi alieteuliwa endapo ataenda kinyume katika kugawa mali, mfano kampa mototo wake nyumba ambaye hakustahili na Hakimu akapitisha shauri lile. Hatua gani zifuatwe kupinga?
Ni kuomba mahakamani kuondolewa kwa Msimamizi wa Mirathi kwa sababu uliyoisema. Na Msimamizi mpya ataomba kuteuliwa. Faili la mirathi halifungwi
 
Lakini akija msimamizi mwingine itasaidia nini kama hiyo mali aliokwapua(nyumba) haijarudishwa. au yeye atapanga upya. lakini mgao ulikubarika kasoro hicho kipengere. swali langu linajikita zaidi kwa tukio la kweli. kuna kisa nimekifungulia thread jana yenye kichwa " msimamizi wa mirathi amgawia mwanae nyumba kinyume na utaratibu hakimu apitisha shauri NI SAWA? " kisa kamili kipo pale;
 
Soma na uelewe nilichosema hapo juu
 
Back
Top Bottom