Msaada wa sheria jamani............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa sheria jamani............

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by NEGLIGIBLE, Mar 23, 2011.

 1. NEGLIGIBLE

  NEGLIGIBLE JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa mfano mimi nimejenga nyumba na nikaipangisha kwa mtu halafu likatokea tatizo kwenye hiyo nyumba;labda kuungua moto kulikosababiswa na uzembe wa mpangaji; wakati ambapo kwenye mkataba wa upangaji hakuna kipengele kinachozungumzia cases kama hizo,nani anakuwa responsible?Na anabanwa kwa kipengele gani?Kumbuka nyumba husika haina bima.
   
 2. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu negligible kwanza inaonekana hujapatwa na hili tatizo ila unataka kujua kama ikitokea uchukue hatua gani zinazositahili.Ikiwa hivyo ndivyo basi utakuwa na mda zaidi wa kuendelea kutafiti juu ya suala lako au umesha tafiti tayari.
  Kwa uelewa wangu mdogo najua suala hili litaangukia chini ya sheria za madhara(law of Negligence) katika sheria hizi huwa haitegemei upande wa pili kama mlikuwa na mkataba naye au la.Vitu ambavyo utatakiwa kuthibitisha ni je,huyo mtu alikuwa na wajibu ambao alitakiwa autekeleze,na je huo wajibu hakuutekeleza na matokeo ya kuto tekeleza ndio yamekusababishia madhara wewe.Kama utakuwa unauwezo wa kuthibitisha hayo unaweza kupeleka madai yako.

  Lakini haya ni mambo ya kimahakama zaidi ambayo si vizuri kukimbilia haraka pale tatizo linapotokea unaweza kuwasiliana kwanza na mhusika si ajabu yeye mwenyewe akawa ameshatambua uzembe wake na akawa tayari kukulipa uhalibifu uliotokea na au mkajadiliana kwa namna fulani ya kuchangia gharama.
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu nafikiri kwenye mkataba wowote wa upangishaji wa nyumba huwa kunakuwa na majukumu ya kawaida kwa mpangaji. Majukumu mengine yanatambuliwa kisheria hata kama hayakuwekwa kwenye makataba. Ningetegemea kwenye mkataba kuwe na kipengele cha "responsible use of the property". Halafu unaposema nyumba kuungua moto, ina maana nyumba yote imeungua?
   
 4. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sheria hazijaweka bayana lakini ukweli hivi vitu vinatokea hasa kuunguza nyumba kweliu kunajamaa yangu ilisha mtokea ila ustaalabu ndio ulitumika maana walipoenda kwenye sheria ikaonekana hakuna sheria inayomwazibisha diirect kwa kuwa watoto ndio walisababisha kuuigua kwa nyumba ila jamaa mwenye watoto aliomba kumpatia fidia mwenye nyumba kwa sehemu fulani yakaisha. mimi naona kuwepo nasheria iliyo direct kutoa mkanganyiko wa kisheria
   
Loading...