Miaka ya 1980 nikiwa mdogo nilitokea kupenda nyimbo nyingi tu kama Bonoonoonoos na Train to Skaville za Boney-M, Hello Africa (Jambo bana ba Afrika) wa Eddy Grant, Girls just want to have fun wa Pat Benatar, D.I.S.C.O. wa Ottawan, One for you, One for me wa La Bionda, Mistery Lady wa Billy Ocean, Tide is High wa Blondie, She works hard for the money na Unconditional love za Donna Summer, There it is wa Shalamar, Body na pia Shake your body (down to the ground) za The Jacksons, What do I do wa Phil Fearon & Galaxy, 20/20 wa George Benson, Celebration na Let's go dancing za Kool & the Gang na nyinginezo nyingi.
Katika kipindi hicho pia palikuwepo nyimbo mbili ambazo ndani yake kulikuwa na maneno ya kiswahili lakini sikubahatika kujua majina ya hizo nyimbo na waimbaji wake ambao kwa aina ya uimbaji na utamkaji wa maneno naona hawakuwa waswahili.
Wimbo wa kwanza ulikuwa na maneno haya "wazimu, wanakuja, wanakuja, wazimu, wanakuja!" wimbo una midundo ya Rock n' Roll.
Hayo maneno yanakuwa yanatamkwa tu bila kuimbwa na mtu aliye kama ana hofu aliyemwona mwenda wazimu na hivyo kupiga kelele kuomba msaada.
Wimbo wa pili una maneno yasemayo " Bibi yangu atazala mtoto, atazala mtoto mwanamke, bibi yangu..... oooooh...nali.... ninalia......oooh ....nali....".
Basi wadau naomba msaada wenu ili nijue majina ya hizo nyimbo na pia walioziimba.