Bahimba
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 510
- 346
Jamani naombeni kusaidiwa namna ya kuweza kuanzisha kanisa, nimeona na kujirizisha pasipo shaka kua makanisa yanalipa, naangalia kipindi hapa kupitia star tv, kuna waumini wanatoa ushuhuda hapa wameniacha hoi, mmoja wa waumini katoa ushuhuda kua last week alikwenda kwa mtumishi huyo kusali, na alipofika pale ukifika Muda mtumishi akaomba watu wenye shida wapite mbele, muumini huyo akapita, mtumishi akamuuliza una shida gani, muumini akamwambia anashida sana maisha ni magumu sasa hata uhakika wa kula yeye na familia yake hakuna, mtumishi akaomba alipo maliza kuomba yule muumini akasikia sms kwenye sim yake, akashangaa kuona m. Pesa imeingia Milioni moja, bila kujua imetoka wapi.