Msaada wa mbinu za kuachana na mpenzi wako mnayefanya kazi pamoja

Tuchki

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
1,740
1,435
Habari za leo natumai wote ni wazima, poleni na majukumu. Jaman ndugu zangu yamenifika hapa na hii ni baada ya kuwa na mahusiano na mfanyakazi mwenzangu ambae tupo wote pamoja katika taasisi fulani.

Ipo hivi huyu mwanaume tulipoonana Kwa mara ya Kwanza kila mtu alimpenda mwenzake lakini sikufanya papara ya kuanzisha mahusiano kwani nilisubiri aanze kuonesha interest yeye, kwa kuwa yeye ni mwanaume kwani niliamini nikianza kumtongoza Mimi itanigharimu

Basi haikuchukua muda mrefu kwani mapenzi hayajifichi baina ya watu ilibidi aniambie kuwa ananipenda hivyo nikajikuta nimeingia kwenye mahusiano naye huku tukipeana ahadi ya kuja kufunga ndoa.

Tatizo linaanza hapa, huyu mwanaume ameshajifahamu kuwa yeye ni mzuri na wanawake wengi wanamtaka na kumtamani na hata kabla sijawa naye kuna wanawake walikua wakimtaka kimapenzi lakin aliwapotezea

Sasa kama mwezi mmoja umepita nimegundua kuwa kuna mwanamke anampa maneno huyu mpenzi wangu kunihusu Mimi ili tugombane kwani hapo mwanzo alishamtongoza jamaa Na jamaa akachomoa

Ila sasa kama wiki mbili nyuma tulikwaruzana na huyu mwanaume ghafla nikaona kaanza kuwa na ukaribu na huyo mwanamke na ukizingatia wote tupo sehemu moja ya kazi na watu wanafahamu uhusiano wetu ko ikabidi nimuulize mpenzi wangu kulikoni naona kawa mkali na hataki kunipa ushirikiano

Kwenu JamiiForum najua humu kuna watu wazima na wengine wengi ambao wamepata changamoto mbalimbali naombeni mnipe ushauri nifanyaje ili ninusuru hili penzi na kama nitashindwa kunusuru penzi basi walau mnipe msaada wa mbinu za kutumia ili nimuachie huyo mwanamke awe na huyo mwanaume pasipo mimi kuumia kwani tupo mazingira ya kazi na muda mwingi tunaonana na mwanamke kaanza kunifanyia visa.
 
Pigania kilicho chako dada.
Mi mwenyewe wife alipigana sana kipind hiko, kipimo chako hiko ndo unajaribiwa hivyo.

Ni chake kwa misingi ipi?hata mume wanakwambia ni wako akiwa ndani kwako akitoka ni wa wote sembuse mpenzi

Tuchki kama ushaanza kuona mwanaume haeleweki achana nae mara moja,kuumia kupo,breakup huwa inaumiza....utaumia lakini muda utakuponya
Usipoangalia utapoteza kazi na mwanaume humpati

Siku zote ni ngumu sana kudeal na kiumbe kisicho na msimamo!!atakusumbua huyo hata mkifika ndoani
 
Dah asante joanah tatizo linakuja jinsi ya kuweza kuishi nao kwani tupo sehemu moja ya kazi tunaonana mda mwingi Na huyo mwanamke anaenifanyia vituko tupo wote kitengo kimoja na Mimi nataka kua na amani yangu moyoni niendelee na maisha yangu joanah,
 
Dah asante joanah tatizo linakuja jinsi ya kuweza kuishi nao kwani tupo sehemu moja ya kazi tunaonana mda mwingi Na huyo mwanamke anaenifanyia vituko tupo wote kitengo kimoja na Mimi nataka kua na amani yangu moyoni niendelee na maisha yangu

Hapo ni either ujitahidi kumind your business ama kuquit hiyo kazi

Ambapo kwangu mie kumind my business ni best option japo najua nitaumia sana kuendelea kuwaona lakini the more unawaona kila siku ndio unazidi kuwazoea hadi kupotezea

Kuquit ni mbaya kwasababu utakuwa umepoteza sababu ya 'ujinga ujinga' wa mtu mwingine ambapo kuna usemi pia wa 'winners don't quit'

Kitendo cha kumuacha huyo mwanaume aende tayari wewe ni winner...endelea kufanya kazi zako,ukiumia lia ama fanya vile unafanyaga kuondoa maumivu...ipo siku utapoa na kupata atakayekufaa zaidi.....kuwa na imani
 
Mtafute Ebitoke akupe tips, yeye amefanikiwa katika hilo kwa kum jonsina mwanamke alieingilia penzi lake kwa baharia....lol!😂😂😂

Bila shaka mambo yataenda sawia kabisa.

Ila kingine jifunze kuacha kuwa controlling kind of woman ili uweze kudumu na ma baharia kwenye mahusiano. Sura mbovu af kibonge hulipi unataka kuleta u much knows?

Huwa hatupendi wanawake controlling kabisa maana kwa kitendo ulichofanya cha kutikisa kiberiti ulitaka jamaa akimbwela uanze kumuendesha utakavyo wakati hulipi! Utaishia kuumia tu hivyo hivyo.
 
@Extrovert,a uanze kumuendesha utakavyo wakati hulipi! Utaishia kuumia tu hivyo hivyo.[/QUOTE]
 
pole dada, chakufanya mwandikie ujumbe kua nakupenda sana bt huwezi share mapenzi hivo kiroho safi unamtakia maisha mema, then utaona atakachojib bt akionesha kukuhtaj mpe masharti
 
Hii itafanya kazi kweli sio kwamba atavimba kichwa maana kuna siku alisema yeye wanawake wanampenda sana, nahisi nikiforce ataniumiza sana
pole dada, chakufanya mwandikie ujumbe kua nakupenda sana bt huwezi share mapenzi hivo kiroho safi unamtakia maisha mema, then utaona atakachojib bt akionesha kukuhtaj mpe masharti
 
Dadaangu utaachana na wangapi? Wew ndo unayejua kama huyo mwanaume anakupenda kweli au mzinguaji migogoro ipo tu na hakuna mwanaume mkamalifu. Ikiwa kimbilio lako ni kuvunja mahusiano kila mnapogombana na mpenzi wako utavunja mahusiano mengi. Umesema mwenyew kwamba anapewa maneno mabaya kukuhusu pigania penzi lako. Ila kama ushamuona jamaa mzinguaji tu achana nae husipoteze muda wako
 
Huu ushauri muonyeshe huyo jamaa.

Golden rules kwa mwanaume ni kutoanzisha uhusiano au kusex na jirani au mpangaji mwenzie.

Kutoanzisha au uhusiano au kusex na workmate.

Kutoanzisha uhusiano au kusex na rafiki wa mpenzi wako, wa mdogo wako au wa Dada yako.

Kwako wewe binti mi naona acha kazi tu. Kwani sh ngap?
 
Mapenzi bwana

Ni zawadi tata kweli

Unaweza kufungua ukauta sio uliyo tegemea


Hapo we jaribu kutafuta suruhisho na mpenzi wako sisi huku tutajaa pm bure kujifanya tunaweza kumbe tutakuharibia


Chukua muda wa kuzungumza nae

Maana wanawake hampendani ndio maana mkichukuiliana wanaume lazima ivume

Mwanaume anaweza kula demu wa mshikaji na wasijulikane
 
Tuchki Huyo joanah anakudanganya. You don't give up easily like that. Huyo ni mpenzi wako, mpaka umeomba Ushaur humu you have feelings for him ambazo joanah hana Ndio maana kirahisirahisi anakuambia umuache. Joanah inaonekana ana stress za mapenzi Ndio maana Mara nyingi anashauri kwa jazba na mihemko. Nadhani ameachwa. Seat with the guy and talk to him ,tell him how much his actions and attitude is hurting you, tell him you love him, tell him what he is doing is not right. Mwambie kwa sauti ya upole sana.
 
Back
Top Bottom