Msaada wa Mawazo wanabodi nimedsco chuo.

Pole fanya mpango uombe upya kwa course nyingine lkn, inawezakuwa hapo hapo UDSM au vyuo vingine achana na kuappeal kama unajua kabisa ulifeli mwenyewe hukufelishwa. Kila rakheri mkuu kumbuka tu one step at a time ,ushike mambo mawili kwa wakati mmoja, shule shule mengine baadaye.
 
Pole sana... ulikuwa unasoma kozi gani iliyopelekea hivo. Suala hilo ni jambo la kawaida kwa maisha ya kusoma ila suala la kuappeal na kuchomoka inategemea na kozi uliyokuwa unasoma. Appliction ndo zinaishia hivo unaweza kufanya process na kuwahi kuomba tena.
 
Haya mambo hayamkuti Mnyama, Young Bro mimi nasoma udsm naingia Mwaka wa 4, nilishakoswa koswa kudisco japo si swala la GPA..
Dogo watu watakushauri kuwa mjasiriamali ila kwangu na wewe bora wa kesho si idea nzuri, Fanya kuapply hapo hapo au chuo kingine.. ku appeal mdogo wangu kwa Jinsi ninavyoijua udsm watakuchinjia mbali.. Apply!
 
Appeal yako itajibiwa kuwa "appeal rejected" so kwa kuwa umri wako bado mdogo me nakushauri apply chuo upya.. Huku mtaani. Mambo ni magumu sana.
 
Umevuna ulichokipanda wee angalia mwenyewe kilimo kinahitaji elimu na ujasiri,chuo unadisco kivipi kama ulikua seriuz au family matters unge postpond kama haukua mkao wa elimu
 
Pole sana. Ulikuwa unasoma kozi gani? Achana na chuo. Neda pale NIT ukasomee udereva wa magari ukishapata class C yako ya VIP unaweza ukapata kazi nzuri na ndani ya mwaka ukawa mbali kuliko hao uliowaacha chuo.
 
Una disco vipi chuo? Tena udsm? Sasa ingekua SUA ingekuaje? Alafu ukute ulikua unasoma kozi za arts au education!!

Ukijiloga kuapply utapotezo muda wako maana ushakiri ulifeli kwa uzembe wako! Mtaani usithubutu kugusa maana jiwe kaharibu kila kitu...

Fanya fasta apply kozi ingine hapo hapo udsm uanze upya... Shukuru ume disco mwaka wa kwanza unge disco mwaka wa tatu au nne ndio ungetia akili!!
 
Acha urongo wewe unadhani Sua ndo chuo kigumu sana!? Unaijua departmental gpa ya Conas wewe? Watu wanadisco na migpa mikubwa tu pale kisa departmental gpa
 
Kama umefeli UDSM huwezi faulu popote, hivyo nakushauri ufanye mambo mengine kuokoa muda, kusoma kupo tu. Ingia informal sector upige pesa
Ila watu humu kichwani kama hazipo vile kwa hyo mtu anafeli Bsc udsm atashindwa CBE wanaosoma simultaneous equations chuo kikuu sasa kwa taarifa yako kuna mtu alidisco tena Duce akakimbilia CBE aliibuka ni best student yupo Bot now
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…