Msaada wa mawazo tafadhali

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
360
386
Pokeeni salamu zangu za dhati ndugu zangu wapambanaji wenzangu na polen na majukumu ya kutwa nzima ya Leo.

*Mimi ni kijana niliyetoka katika familia duni na isiyo jiweza kiuchumi lakin Nina ndoto za kufuta historia ya ya umaskin katika familia yangu kwa siku za mbeleni.

Kwa maana hiyo ni lazima nipambane kw bidii na juhudi pamoja na nidhamu ya Hali ya juu, nina wazo kuna idear ya jambo Moja nadhani nikifanikisha nitatoboa kwa urahisi. Nataman ninunue eneo la heka Moja kwa makadirio ni umbali wa km 6 kutoka Arusha mjini.

Baada ya kununua
  • Nifuge nguruwe 50 na kuku wa mayai 1000
  • Sungura, Bata aina zote, njiwa, simbilisi mbuzi
  • Na ng'ombe wa gredi Kama 3
  • Kwa muda wa miaka 3 Nina huhakika wa kurudisha hela na na faida juu hata Kama mambo yatakuw tofauti na wazo langu.

Changamoto ni kwamba Sina mtaji na kwa project yangu Hadi kuanza kutengeneza faida nahitaji kias Cha million 16 je nazipataje?

Kuna mtu namtegemea,
  • Sijui nitumie mbinu gani kuandaa project yangu
  • Ili nikimpelekea aweze kuniunga mkono
  • Au taasiai yake iniunge mkono
  • Ndio maana nipo hapa
Naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kuandaa project yangu na ni vitu gani vya kuzingatia?
Naomben wataalamu mnisaidie kwa hili.

Mbarikiwe sana.
 
Tengeneza kikundi kisha sajili na mfungue account. Baada ya hapo hayo mawazo yako yaweke katika maandishi na nenda kwa afisa maendeleo ya jamii wa kata akupe muongozo kuhusu 10% ya halmashauri
 
Tengeneza kikundi kisha sajili na mfungue account. Baada ya hapo hayo mawazo yako yaweke katika maandishi na nenda kwa afisa maendeleo ya jamii wa kata akupe muongozo kuhusu 10% ya halmashauri
Asante sana
Je tunatakiwa tuwe vijana wangapi?
Vip kuhusu usawa wa jinsia?
Naomba ufafanuzi kidogo
Pia unafahamu kikundi chochote ambacho kilifanikisha hili jambo?
 
Asante sana
Je tunatakiwa tuwe vijana wangapi?
Vip kuhusu usawa wa jinsia?
Naomba ufafanuzi kidogo
Pia unafahamu kikundi chochote ambacho kilifanikisha hili jambo?
Vijana kuanzia watano mwisho kumi mkizidi hapo itakuwa fujo. Umri wa vijana ni kuanzia 18 mwisho 35, usawa wa jinsia haizuii kufanya mkakosa ila kama mnaweza wawepo. Unaweza mkachanganya wakinamama hawaangaliwi umri hawa.
Vingi sana lakini inategemeana pia na halmashauri uliyopo kwa huko na uwaledi wa mkurugenzi wenu, afisa maendeleo ya jamii wilaya na madiwani wenu wa huko
 
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom