Msaada wa Mawazo tafadhali

Venas_Hb

New Member
Jul 20, 2021
3
1
Msaada wa Mawazo

Nimemaliza Form 6 mwaka juzi ila nikaona nijiegeshe katika baishara kwa muda, kwa sasa nafanya kazi ya kusajili laini za simu mitaani (Freelancer) ila naona Tayari nimeshaanza kuchoka, Ila Mpk sasa Nina akiba yangu ya Shilingi laki saba (700,000), lengo la kupost humu Ni kutafuta jinsi gani ntaweza kuizalisha hiyo pesa niliyonayo na kuleta faida mara dufu.

WAZO LANGU, pamoja na lengo langu

Nilikua nafikiria Nianze na biashara ya Kuuza Boska za kiume, Sidiria, Taiti za wadada, Pamoja na Chupi za kike.

Au

Nianze nitafute eneo mahala la kukodisha, kisha nianze Kufuga kuku wa kienyeji pamoja na Briola.

Je! Nibiashara ipi inayolipa vizuri, licha ya changamoto za kawaida??

Sihitaji matusi, wala Comment za kukejeri please
 
Pia unaweza waza kwenda karume Asubuhi kupoint viatuu,
Viatu ni bidhaa inayouzika sanaa hata zaidi ya nguoo.
 
Kuna biashara ya uzalishaji natarajia kuianzisha,nimeshafanya tafiti kadhaa za hapa na pale kuihusu,sasa nahitaji vichwa vyenye taaluma kadhaa ambazo zinaweza kunisaidia kukamilisha plan yangu,watu ninaowahitaji ni wale wenye uelewa mzuri kwenye kemia(chemistry) biolojia( biology) na marketing,biashara yangu haitahitaji mtaji mkubwa sana hivyo hawatahitajika kuchangia gharama za uanzishaji wala uendeshaji wa biashara,watakachohitajika kuwa nacho ni ushauri na msaada wa kitaalamu utakaoweza kusaidia kwenye uzalishaji,uboreshaji,na masoko,hivyo kama wewe unadhani una kigezo chochote kati ya hivyo tafadhali usisite kuwasiliana na mimi kwa Email yangu @Elijahlema44@gmail.com karibuni sana tujikwamue,kwa pamoja tunaweza.
 
Back
Top Bottom