Msaada wa mawazo na ushauri

Binadamu tukubali kukutana na changamoto jaman..bila changamoto hujaishi...utachanjwa michale mwili mzima na utazidi kudorora...barabara yenyewe ina kona ...lol
Kiukweli chale na haya mengine hapana na hicho ndio chanzo cha kuachwa nipigane mwenyewe, ila huenda wapo watu wanaweza kukuvusha kwakuwa Mungu kawafanya sababu
 
Usifikirie hayo madude .dah..mm hapana aisee hata kama sina imani nitalia na Mungu atanionesja njia..amini ni changamoto tu hizo
 
Ogea chumvi ya mawe kwa mwezi mmoja utakuwa poa, ama mkoa na usiage mtu anza mapambano upya kuna ndugu zako wanakuchezea
Hii ni moja ya tiba nzuri mno dhidi ya nguvu zozote hasi,ukishakoga unachukua maji masafi unaweka chumvi yako ukijitakasa,jitahidi kusema neno wakati unajimwagia maji ya chumvi,lolote ambalo linaendana na changamoto zako linalolenga kuleta suluhisho.
Kubwa zaidi amini Mungu anaweza yote,kwa imani yako,mrudie yeye na shikamana nae katika yote.

Usiogope kuanza upya chief,maisha yako,dhamana yake umebeba wewe,hata kama dunia nzima itakuwa against na wewe,usijichukie,jipende mwenyewe,ipende familia yako zaidi.
Pole sana,naamini utashinda.
 
My friend.... You will prosper.

Mungu hufanya njia pasipo na njia....you will Rise again...

We shall never be defeated....NEVER

Mwenyezi Mungu huipa Ardhi afya Tena Baada ya miezi ya ukame Hata ukipiga jembe unaumia.. but Mvua hunyesha na Ardhi huotesha mimea..

Mungu huyo huyo atakufanya uchipue TENA... Mimi sijakata Tamaaa wewe usikate Tamaaa....
 
Chumvi ya mawe ni hii inaitwa Epsom salt au nyingine?
 
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu, Mimi ni kijana umri miaka 33.

Nimefanya kazi kama Mwalimu wa Sekondari kuanzia 2012 mpaka mwaka 2019 baada ya kupata fursa ya kwenda kujiendeleza kielimu nchini Marekani kuanzia January 2020.

Katika kipindi cha miaka hiyo 7 nikiwa kama Mwalimu nimepitia mambo ambayo mwanzo sikuwahi kuamini kama ni kweli au ni mapito madogo tu. Hapa nilihisi labda cheo changu kwani hapa nilibahatika kiukweli kuaminiwa na kuwa makamu katika taasisi kubwa mno na pia kusimamamia miradi mingi ambayo ilinisaidia kusafiri nchi mbalimbali. Nilijiona mwenye bahati na sijawahi kuwa tatizo kwa niliowaongoza.

Kwanza nilipoteza uoni wa jicho langu moja, pia kupata maumivu ya mwili mara kwa mara bila kujua chanzo chake hata pale nilipoenda hospital.

Nikiwa kazini nilianza kuandamwa na ajali japo sikuona ni tatizo kubwa katika maisha. Mwisho nikapata ajali mbaya nikiwa njiani kuelekea mkoani kuichukua familia yangu, kwa mapenzi ya Mungu nilitoka salama bila jeraha ila abiria niliokuwa nimewapa msaada walipata majeraha makubwa na wakaja kuzinduka baada ya mwezi.

Hapa nilipata mstuko kwani nilipelekwa mahakamani na kwa mshangao kesi ilichukua mwaka na nusu bila kuisha kwa madai wale majeruhi wanadai fidia na hapa nafikri polisi walijawa na tamaa ya hela.

Baada ya matukio hayo nikaaza kupata mitihani mizito tena, watoto wangu nao wakaanza kupata ajali za moto, kiasi kwamba muda mwingi nikautumia kwenye kuhangaika kutibu watoto na mimi mwenyewe.

Kitu kilichonisukuma kuandika hili ni hali ninayopitia baada ya kurejea Tanzania katikati ya mwaka 2020, Kila nilipojaribu kutafuta kazi ya kufanya nilijikuta mgonjwa, nikikaa nyumbani siiumwi kitu.

Nilijaribu kuacha kuhangaika kutafuta kazi hizi zinazohitaji taaluma yangu kwa hofu ya labda husda nijikite kwenye kazi ndogo ndogo kama kilimo, ufugaji au hata uvuvi, ila baada ya watu kuniona huko yanatokea mauzauza tena na lazima nipoteze kila kitu mpaka hata hela ya kula inaisha yote na hapo utapata taarifa watoto wanaumwa.

Kibaya zaidi nimetengwa na familia yote baada ya Mimi kugoma kujiingiza kwenye mambo ya kuamini kuwa nimerogwa, naweza amini hivyo ila sijaona kuwa suluhisho ni mimi kwenda kwa waganga.

Pia wengi wanaamini nimechanganyikiwa kutaka kufanya kazi kama kilimo au biashara ndogo wakifikiria nimetoka Marekani na nimesafiri sana iweje nisifanye kazi za ofisini kama akili ipo sawa? Binafsi hilo halinisumbui na sitaki kuamini kuwa lazima niwe ofisini kabisa.

Pia katika kipindi nikiwa vizuri nilikuwa na kundi kubwa mno la marafiki ambao nilijitoa kwao mno ila hapa ninaposema hata simu hazipokelewi labda wanahisi nataka kuwaomba hela. Hali hii imeniweka katika hali ngumu mno nisijue nianze na lipi nimalize na lipi.

Najaribu mno kutoka nilipo ila naanguka tena. Kwasasa ninaomba kama kuna mtu amepitia hali hii na alitokaje katika hili ajaribu kushauri, pia msaada mkubwa ninaoomba kwenu ni kama yupo mtu atahitaji tufanye kazi nitakuwa tayari huenda itasaidia mno, binafsi mwenyewe nahisi siwezi tena kwani hata mtaji wote umeteketea kwa kuilisha familia na matibabu wakati siingizi kitu.

Pia nitakuwa tayari hata kuishi porini kufanya kazi ili tu niokoe familia yangu.

Natanguliza shukrani zangu.
Pole sana mkuu.
 
Pole sana mkuu,
Kwanza chagua upande wa iman
Pili fanya maombi ya kupinga vifungo vyote vya shriki, vijicho, n.k
Kama umewah zur mtu kwa vyovyote tubu
Kiukweli nimejiweka karibu na Muumba wangu, pili sijawahi hata kwa makusudi kumdhuru mtu au kumuumiza, hata kazini sijawahi kuwa kuburi au kikwazo kwa mtu yoyote hilo nasimama kulisema ila binadamu hatuwezi kuwa wakamilifu. Ninachofahamu nishawahi kupata vikwazo baada ya kupewa majukumu makubwa tofauti na umri wangu na katika niliokuwa nawaongoza ni labda wawili tu ndio nimezidi umri wote ni wakubwa kwangu.
 
My friend.... You will prosper.

Mungu hufanya njia pasipo na njia....you will Rise again...

We shall never be defeated....NEVER

Mwenyezi Mungu huipa Ardhi afya Tena Baada ya miezi ya ukame Hata ukipiga jembe unaumia.. but Mvua hunyesha na Ardhi huotesha mimea..

Mungu huyo huyo atakufanya uchipue TENA... Mimi sijakata Tamaaa wewe usikate Tamaaa....
Shukran sana mkuu, naamini nitasimama na Mungu yupo kwani yapo mengi alinipa bila kumuomba.
 
Una option mbili tu kutegemeana na imani yako, sijui wewe ni dini gani, kama ni Mkristu nenda kwa Yesu; tafuta makanisa ya kweli ya kiroho, au dhehebu lako unalosali hivi sasa, ongea na kiongozi wako wa kanisani mueleze yote yanayokutokea ukiamini yatakwisha, atakufanyia maombi.

Option ya pili; kama mambo ya dini hayapandi sana nenda kwa wazee wako ulipotokea (kijijini kwenu) waeleze hali yako watajua cha kufanya, niliwahi kutana na mtu akaniambia mtu akiwa mjini hata apatwe na tatizo gani, akirudi alikozaliwa kuwaeleza lazima hilo tatizo litakwisha, kwasababu mizimu ya kwenu inakufahamu kila unachofanya, unachopitia, na ulichokutana nacho, hivyo inazo dawa zako. Hili nililiona baada ya marafiki wawili waliougua kichaa huku mjini kwenda kwao na wakapona kabisa.

Fanyia kazi hizo shauri mbili hapo utarudi kwenye hali yako ya kawaida, utakuwa umechezewa kazini kwako au na ndugu zako wanaokuonea wivu kutokana na mafanikio uliyokuwa nayo, amka sasa kairudishe neema yako.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu, Mimi ni kijana umri miaka 33.

Nimefanya kazi kama Mwalimu wa Sekondari kuanzia 2012 mpaka mwaka 2019 baada ya kupata fursa ya kwenda kujiendeleza kielimu nchini Marekani kuanzia January 2020.

Katika kipindi cha miaka hiyo 7 nikiwa kama Mwalimu nimepitia mambo ambayo mwanzo sikuwahi kuamini kama ni kweli au ni mapito madogo tu. Hapa nilihisi labda cheo changu kwani hapa nilibahatika kiukweli kuaminiwa na kuwa makamu katika taasisi kubwa mno na pia kusimamamia miradi mingi ambayo ilinisaidia kusafiri nchi mbalimbali. Nilijiona mwenye bahati na sijawahi kuwa tatizo kwa niliowaongoza.

Kwanza nilipoteza uoni wa jicho langu moja, pia kupata maumivu ya mwili mara kwa mara bila kujua chanzo chake hata pale nilipoenda hospital.

Nikiwa kazini nilianza kuandamwa na ajali japo sikuona ni tatizo kubwa katika maisha. Mwisho nikapata ajali mbaya nikiwa njiani kuelekea mkoani kuichukua familia yangu, kwa mapenzi ya Mungu nilitoka salama bila jeraha ila abiria niliokuwa nimewapa msaada walipata majeraha makubwa na wakaja kuzinduka baada ya mwezi.

Hapa nilipata mstuko kwani nilipelekwa mahakamani na kwa mshangao kesi ilichukua mwaka na nusu bila kuisha kwa madai wale majeruhi wanadai fidia na hapa nafikri polisi walijawa na tamaa ya hela.

Baada ya matukio hayo nikaaza kupata mitihani mizito tena, watoto wangu nao wakaanza kupata ajali za moto, kiasi kwamba muda mwingi nikautumia kwenye kuhangaika kutibu watoto na mimi mwenyewe.

Kitu kilichonisukuma kuandika hili ni hali ninayopitia baada ya kurejea Tanzania katikati ya mwaka 2020, Kila nilipojaribu kutafuta kazi ya kufanya nilijikuta mgonjwa, nikikaa nyumbani siiumwi kitu.

Nilijaribu kuacha kuhangaika kutafuta kazi hizi zinazohitaji taaluma yangu kwa hofu ya labda husda nijikite kwenye kazi ndogo ndogo kama kilimo, ufugaji au hata uvuvi, ila baada ya watu kuniona huko yanatokea mauzauza tena na lazima nipoteze kila kitu mpaka hata hela ya kula inaisha yote na hapo utapata taarifa watoto wanaumwa.

Kibaya zaidi nimetengwa na familia yote baada ya Mimi kugoma kujiingiza kwenye mambo ya kuamini kuwa nimerogwa, naweza amini hivyo ila sijaona kuwa suluhisho ni mimi kwenda kwa waganga.

Pia wengi wanaamini nimechanganyikiwa kutaka kufanya kazi kama kilimo au biashara ndogo wakifikiria nimetoka Marekani na nimesafiri sana iweje nisifanye kazi za ofisini kama akili ipo sawa? Binafsi hilo halinisumbui na sitaki kuamini kuwa lazima niwe ofisini kabisa.

Pia katika kipindi nikiwa vizuri nilikuwa na kundi kubwa mno la marafiki ambao nilijitoa kwao mno ila hapa ninaposema hata simu hazipokelewi labda wanahisi nataka kuwaomba hela. Hali hii imeniweka katika hali ngumu mno nisijue nianze na lipi nimalize na lipi.

Najaribu mno kutoka nilipo ila naanguka tena. Kwasasa ninaomba kama kuna mtu amepitia hali hii na alitokaje katika hili ajaribu kushauri, pia msaada mkubwa ninaoomba kwenu ni kama yupo mtu atahitaji tufanye kazi nitakuwa tayari huenda itasaidia mno, binafsi mwenyewe nahisi siwezi tena kwani hata mtaji wote umeteketea kwa kuilisha familia na matibabu wakati siingizi kitu.

Pia nitakuwa tayari hata kuishi porini kufanya kazi ili tu niokoe familia yangu.

Natanguliza shukrani zangu.
Matatizo yako ni madogo Sana Kama tu ukakabidhi maisha yako kwa Kristo. Yeye atakuwekea ulinzi, atalinda mali zako zote, familia yako na kukutimizia mahitaji yako yote hata usiwe mhitaji tena.

Yesu akasema, "yote yawezekana kwake aaminiye"

"God is all you need to have all your need mets, faith is all required to allow God to take action into your life and understanding of his word is all required to make your faith alive"
 
Pole sana,Mkuu nguvu za Giza zipo na zina Fanya kazi kwa ufanisi sana ndugu yangu,ngoja nikupe mfano Wa mtu aliyeharibu Maisha ya baba Yangu mzazi.

Mzee wangu alikuwa reporter Wa Radio Tanzania miaka ya 70 hivi,baadae mhariri Wa gazeti moja lililokuwa linamilikiwa na serikali,katika kuugua kwake ilianza kama mzaha,alipopangiwa shift za mchana yeye alienda usiku na kinyume chake pia,ameendelea hivyo na alikuwa mtu Wa dini sana mwisho Wa siku alifukuzwa kazi na kuamua kurudi kijijini maana ilifikia kipindi akawa anataka kukimbia uchi.

Baada ya kurudi nyumbani kwa wazazi wake ambao ni babu na bibi zangu walijaribu kumpeleka kwa wataalamu Wa tiba asilia, alikuwa mjuaji sana,alidai mganga mkuu ni yesu tu,japo alipata unaafuu kwenye miaka 80 akapata kazi lakini nayo hakuifikisha mbali akawa ametimuliwa ,familia iliyumba maana alitegemewa katika kuendesha familia,mwisho Wa Siku mama aliondoka na familia ilivurugika kabisa,lakini chanzo cha yote ni roho wabaya aliotupiwa baba Yangu huko pwani kutokana na wivu Wa waswahili

Mzee wangu amekuja kufariki utadhani hakuwahi kuwa mtu msomi na mtumishi Wa serikali,kiufupi chanzo haya yote ni nguvu za giza.

Roho wabaya wanapo mwingia mtu huwa wanamletea ujuaji Fulani ,watu Wa nje wanakuona kabisa kuwa mwili wako hauko sawa ila wewe kuwakubalia inakuwa ngumu,ni sawa na mwanamme aliyelishwa limbwata,watu wote wanaomzunguka hutambua kabisa kuwa kalishwa limbwata ila akiambiwa huwa anakuwa mbishi sana.

Mkuu shetani yuko kazini hajalala,chukua hatua kabla hujapotea,kama ni ushirikina Wa pwani komaa huko huko pwani wautoe,kama ni wabara hangaika huko huko wakusaidie kabla hali haijawa mbaya,pole sana,
 
Ahsante sana mkuu, hizi mambo nimeambiwa sana ila nashindwa nianzie wapi.
Kiukweli nimetokea mazingira ambayo naweza sema Mimi ndio mtu wa kwanza kufika huko duniani na hata kusoma kiwango hicho.
Bahati mbaya nimechelewa mno na ndugu wameniangalia waone mwisho wangu
 
Back
Top Bottom