Msaada wa mawazo kwa rafiki yangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa mawazo kwa rafiki yangu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NasDaz, Oct 3, 2011.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kuna rafiki yangu mmoja alifunga ndoa zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, hivi majuzi alinidokeza kwamba tangu afunge ndoa na mke wake alijisikia furaha ya ndoa katika wiki ya kwanza tu na baada ya hapo hakupata tena kuifurahia ndoa yake. Kwa mtizamo wake ni kwamba ilikuwa ni baada ya hiyo wiki moja ndipo alipokuja kugundua kwamba aliyeoa hakuwa chagua la moyo wake.

  Binafsi, nilishituka sana nilipomsikia akinisimulia jambo hili. Mshangao wangu ulitokana na ukweli kwamba wakati alipokuwa ktk mchakato wa kufunga nae ndoa mimi nilikuwa pamoja nae muda mrefu. Nakumbuka enzi zile alikuwa akija na picha za mchumba wake (mke wake kwa sasa) ofisini! Ilikuwa kila alipopata nafasi, angezichukuwa picha za mchumba wake na kuanza kuziangalia. Angeweza kuzikodolea macho picha hizo hadi robo saa jambo ambalo baadae hata mimi alianza kunikera! Pale nilipomuuliza ni kwanini kila wakati anapenda kuziangalia picha za mchumba wake tena kwa muda mrefu hivyo hadi wakati mwingine alikuwa anaacha kufanya kazi kwa muda kwa kuziangalia picha hizo; jibu lake kila mara lilikuwa ni kv anampenda sana hivyo kila wakati anapenda kumwangalia na haishi hamu kuziangalia picha hizo! Hata hivyo, leo hii ananiambia kwamba ilimchukua wiki moja tu kufurahia ndoa yake jambo lililomfanya amrejee mpenzi wake wa zamani ambae alikuwa ameishi nae zaidi ya miaka mitano! Rafiki yangu amechanganyikiwa na hajui afanye nini hasa ukizingatia kwamba dini yake hairuhusu kuacha mke na yeye bado ni kijana mdogo sana ambae hajafikisha hata miaka 30! Mshikaji wangu huyu aliniomba msaada wa mawazo kuhusu afanye nini, nami nawageukia wana jamvi kutafuta msaada wa mawazo.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu rafiki yako asijitie uzinzi usokua na maana,na kama ameshaoa sasa huyo wazamani anamfatia nini? au sio mwanamme anaeweza kufanya mamuzi? mwambie awache mawasiliano na huyo mchuchu wake wazamani na ajue kua ss ameshakua mume wa mtu uzinzi sio mzuri.
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Let me digest your story first b4 any comment!
   
 4. A

  Andrewgrey91 Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwambie aziangalie picha zile tena may b atampenda tena ka zamani
   
 5. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Uzinzi ukimuingia mtu akirini unakua unatamani uzinzi kila wakati, hii huwa sawa na mwizi aliyezoea hata kama ana m1 bado ataiba 100. Huyo rafiki yako halidhiki hivyo aache tamaa.
   
 6. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote am very sorry with ur friend!!!

  ANGALIZO!!!

  Kwa mtazamo wangu, rafiki yako alishakuwa na mashaka na huyo mke wake tangu kipindi cha uchumba wao tofauti na vile alivyokueleza! Kosa alilofanya ni kutotaka kuzisikiliza na kuyafanyia maamuzi hisia zake na badala yake akahadaika na shere zilizokuwa zinachezwa na macho yake! Chige unashangaa ni kwanini mapenzi yaliisha mapema kiasi hicho wakati zamani alikuwa anashinda akiziangalia picha za mchumba wake ikiwa ni ishara ya upendo!! Ungekuwa makini, hapo hapo ungegundua kwamba tangu zamani rafiki yako alikuwa akijilazimisha kumpenda huyo mchumba wake wakati penzi hilo halikuwapo. Suala la yeye kuwa akiziangalia picha za mchumba wake kila wakati na kwa muda mrefu inaonesha kwamba kuna kitu alikuwa anakitafuta kwenye picha hizo hili kihalalishe penzi lake! Ninachosema ni kwamba; nafsi yake ilikuwa haijapenda hivyo kila wakati alikuwa akiziangalia picha hizo ili apate kitu kitakachoiridhisha nafsi yake! Kwavile alikuwa hakipati kitu hicho kitu, ndio maana ilikuwa ikimchukuwa muda mrefu akihangaika kukitafuta! Pale alipodanganywa na macho yake kwa kuzani amekiona, aliirudisha picha hiyo mfukoni lakini muda mfupi baadae angegundua kwamba BADO!!!! Bado hiyo ingemlazimisha kuzichukuwa tena na tena picha hizo na kuanza tena na tena kukitafuta kitu hicho ambacho mara zote alishindwa kukipata!!! MOYO, haukupenda akawa anatoa kazi kwa macho yatafute kitu kitakachouridhisha moyo huo! Uangaliaji picha unaotokana na mapenzi hauhitaji kuangalia picha kwa muda mrefu kiasi hicho! Nusu dakika tu inatosha kabisa kuiangalia picha ya umpendae kiukweli kv hakuna unachokitafuta kwenye picha hiyo. Huna unachokitafuta kv “everything in tht photo is perfect!” Ukiona unaiangalia kwa muda mrefu na kila wakati basi kuna kitu unakitafuta kutokana na ukweli kwamba kuna conflicting interests kati ya utashi na moyo wako na hivyo unatoa kazi kwa macho kutatua utata huo! Nina kazi nyingi kwa sasa, hard to write. Ni-PM namba yako/yake for advice!


   
 7. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Inawezekana huyo mkewe alimuendea mumewe kwa kalumanzila ili aolewe sasa ndio yameisha hivyo. Maana tunaweza mlaumu mbaba hapa kumbe aliingizwa mkenge
   
 8. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  hahahaha inabidi arudi tena kwa Kalumanzira aongeze muda................kwa nini alikubali ya muda mfupi
   
 9. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  kazi ipo hizi ndio za siku hizi maruweruwe kibao zinaitwa bora ndoa
   
 10. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa yako ananishangaza coz nahic hajatulia kbs, kwann alishindwa kumuoa huyo mpnz wake wa mwanzo alieishi nae kwa miaka mitano, na akaenda kumuoa huyo ambae ni mkewe kwa sasa na kipi tena kimemfanya amchukie baada ya wiki moja na kumrudia yule wa mwanzo,binafsi naona huyo jamaa bado ni wa kiume coz kakimbilia kuoa akiwa hajui anachokihitaji maishan,atulie kwa mkewe aache umalaya!
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  hapo nimekupenda Maty. ila umejuaje, isije ikawa na wewe ni muumini wa mambo hayooooooooo!
   
 12. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Na bahati ni yeye asiyempenda mke, hapo ingekuwa ni mke hampendi mwanaume, mida hii ndoa ingekuwa mchegoni. Mwanamke akishakinai, lazima akutose tu , huwa hawana kuremba hawa viumbe!
   
 13. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  tatizo la jamaa ni kufanya comparison ya mkewe na huyo kipwepwelepwe cha nje ajitahidi kurudisha moyo kwa yf
   
 14. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hahhaaa.....expaya date reached...!!
   
 15. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  kaka,labda ungechelewa kidogo mimi ningepost uzi kama huu kwa asilimia tisini....mimi pia nina rafiki yangu wa karibu sana,mwaka 2009,masaa machache kabla ya send off yeye akiwa ndio mtarajiwa,akinipa habari kama hiyo,sikuamini na nikamwambia acha utani,alisisitiza lakini yakaisha na siku mbili baadaye akafunga ndoa ya kanisani,katoliki!wamekaa na mkewe kama mwaka hivi,wamepata mtoto lakini hivi ninavyoandika,amemwacha mkewe wa ndoa na anataka kuoa mwingine!!mke kahangaika mpaka kwa wazazi wa jamaa,wameshindwa kusawazisha,mimi pia nimejaribu kunusuri hiyo ndoa kwa nafasi yangu,nimeshindwa!!jamaa yuko shinyanga na mkewe wa ndoa yuko moshi......sielewi,nini kinatokea juu ya hali hii,nahisi inaanza kushika kasi,tujadiliane kwa pamoja
   
 16. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kuna mwingine huku yeye hupenda kuangalia mkanda wa video wa harusi yake in a rewind....anasema anapenda anavyokuwa anaaga watu huku akirudi kwenye gari na kuondoka ukumbini
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  asikusumbue na uzinzi wake. Au alipenda photoshop, kuona k2 halisi hamu ikamuisha
   
 18. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hivi umri muafaka wa kuoa ni upi?
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa naona kama ameingia kwenye ndoa mapema mno, bado utoto unamsumbua, mwambie aache tamaa..
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  :smile-big:
   
Loading...