Msaada wa Matibabu kwa Kijana Abel Machanga

Msaada wa Matibabu kwa Kijana Abel Machanga

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,981
Reaction score
4,174
Kijana Abel Machanga mwenye umri wa miaka 24 amelazwa Hospital ya Taifa Muhimbili Wodi ya Sewahaji,chumba namba 19,Kitanda namba 28 kwa tatizo la uvimbe kwenye ubongo ambalo limesababisha macho yake kutoka nje.

Familia inaomba msaada wa wasamaria wema ili kugharamia matibabu ya Abel kutokana kuwa gharama za matibabu ni kubwa kuliko uwezo wa familia.

Kwa yeyote atakayetakayeguswa na taarifa hii, anakaribishwa kumtembelea Abel Hospitalini ili kukutana naye na kusikia kilio chake Kwa mlio mbali, tunaomba misaada yenu kupitia kwa kaka wa Abel Bw. Christopher Machanga kwa namba Tigo 0655 54 56 67 Airtell 0784 54 56 67 Voda 0755 54 56 67

SHIME WATANZANIA, TUJITOE KWA MOYO KUOKOA MAISHA YA MWENZETU NA KUPUNGUZIA MATESO MAKALI ANAYOKABILIANA NAYO KWA SASA.

TUNATANGULIZA SHUKRANI.


Chanzo: Michuzi

 

Attachments

  • 1435834436124.jpg
    1435834436124.jpg
    31.1 KB · Views: 1,394
POLE SANA NDUGU ABELI, TUNAKUOMBEA SANA MOLA AKUPE NAFUU UPESi, NA NINAAMINI U WILL GET WELL VERY SOON INSHALLAH
 
Bwana wetu YESU KRISTO atakuponya katika madhira hayo.
attachment.php
 
Mshukuru Mungu ewe mwana wa Adam kila unapoamka asubuhi na kujikuta uko mzima, pole Abel, Mungu na atusaidie tupate moyo wa kukusaidia
 
Mkuu UMENILIZA Kwa Maelezo Yako Na Picha Ya Huyu Kijana Wetu. Ni Umasikini Tu NILIONAO Mkuu Lakini Kwa Ninavyojijua Nilivyo Na Huruma, Utu Na Ubinadamu Ningekuwa NINAZO Kama Hawa Wawili Wanaotarajia Kufanya MDAHALO Wa UBISHANI Wao Kesho Ijumaa au Kama Yule Wa Pale MATAA Tazara Ningeshamchukua Na Kumpeleka Kumtibia Kijana Wetu Huyo Mzuri Huko Ng'ambo.

Mkuu Hiyo Picha Imenipa Sana HUZUNI Na SIMANZI Na Kweli Sasa Nimeamini Kuwa Kumbe Wewe Ukisema Una Shida Ni Kumkufuru Tu Mwenyezi Mungu Wetu Kwani Wapo Wenye Shida Kubwa Kuliko. Nampa Pole Sana Huyo Mwanangu ( Kijana Mgonjwa ) Na Mwenyezi Mungu Awape Moyo Wa Uvumilivu Wazazi Wake au Waangalizi Wake Na Nina Imani Kuwa Watajitokeza Tu Watu Wenye Moyo Wa Kweli Na Watamsaidia Na Kwa Mimi KAPUKU ( Choka Mbaya ) Nitakachokifanya Ni Kumwombea Tu Kwa MAULANA.
 
Mkuu UMENILIZA Kwa Maelezo Yako Na Picha Ya Huyu Kijana Wetu. Ni Umasikini Tu NILIONAO Mkuu Lakini Kwa Ninavyojijua Nilivyo Na Huruma, Utu Na Ubinadamu Ningekuwa NINAZO Kama Hawa Wawili Wanaotarajia Kufanya MDAHALO Wa UBISHANI Wao Kesho Ijumaa au Kama Yule Wa Pale MATAA Tazara Ningeshamchukua Na Kumpeleka Kumtibia Kijana Wetu Huyo Mzuri Huko Ng'ambo. Mkuu Hiyo Picha Imenipa Sana HUZUNI Na SIMANZI Na Kweli Sasa Nimeamini Kuwa Kumbe Wewe Ukisema Una Shida Ni Kumkufuru Tu Mwenyezi Mungu Wetu Kwani Wapo Wenye Shida Kubwa Kuliko. Nampa Pole Sana Huyo Mwanangu ( Kijana Mgonjwa ) Na Mwenyezi Mungu Awape Moyo Wa Uvumilivu Wazazi Wake au Waangalizi Wake Na Nina Imani Kuwa Watajitokeza Tu Watu Wenye Moyo Wa Kweli Na Watamsaidia Na Kwa Mimi KAPUKU ( Choka Mbaya ) Nitakachokifanya Ni Kumwombea Tu Kwa MAULANA.

Yaani pesa ya Tanzania inafanya kazi kwenye siasa tu, na walioko siasani ndio wanaozila.
Inasikitisha kuona kijana analia ili kutetea afya yake huku watu wengine wakitoa mamilioni ya shilingi kwa shughuli za kipuuzi.
 
"Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Arshi tukufu (akuponyeshe)"AMEEN

Mkuu hembu toa gharama halisi za matibabu
 
Ukijiona mzima shukuru Mungu,hapa Duniani kuna watu wanateseka jamani.
 
Back
Top Bottom