Bebrn,
Wewe kama umesoma database na unaielewa, huna haja ya kujikunja kuandaa maswali na majibu ya interview. Hakuna mwenye interest "kwenye effective interview" kujua unachoju. Interview zilizoenda shule huwa wanapima uwezo wa mtu kufikiria na kufanya maamuzi sahihi.
"Msomi sio anayejua kila kitu kichwani... Bali ni yule ajuaye pa kupata anachokihitaji!"
Mkuu inategemea unakwenda kufanya kazi wapi..na database gani na company ina deal na nini,tangazo la kazi linasemaje...wanahitaji nini hapo...so ni vitu vingi vya kuangalia hata kabla hujaomba kazi hiyo...so utakacho andika kwenye Resume yako mara kwa mara ndio watakacho kuuliza na kama kuna ya ziada kuangalia kama una uwezo wa kufikiri zaidi ya unacho jua na kama uko tayari kupokea vitu vipya.
Wakati mwingine...unaweza kuta wao wana maswali yao..kwa mfano nilisha fanya interview aliye nifanyia alikuwa ana maswali 17 ambayo yalitokana na nilicho andika kwenye CV.Baadhi ya nyakati inabidi uwe na hicho ulicho kiandika kwenye kichwa..bila kufunua CV yako....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.