Msaada wa maneno ya Kiswahili yanayoanziwa na " MWU"

Mtu Kwao

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
394
713
Wanajamvi salam!

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu. Na mtoto wangu anasoma darasa la pili sasa kuna kazi wamepewa yakuandika maneno ya kiswahili yenye maana yanayo anziwa na Mwa, mwe, mwi, mwo na Mwu.

Sasa maneno mengine yote yamepatikana ila sasa neno linaloanziwa na " Mwu "ndo changamoto.

Naombeni enyi watalaamu wa lugha mnisaidie maneno ayo yanayoanziwa na "MWU".
 
MWU ni neno ambalo ni uyeyushaji mbapo herufi W asili yake ni U kavu kwahiyo kwenye uyeyushaji huandikwa W hivyo MWU ni sawa na MUU, au MU kwahiyo hapo tunapata MWUGUZI, kutoka neno muuguzi, tafuta maneno mengine yenye MUU../ MU... na utumie MWU...

Mwalimu umetufunga kamba kidogo kuhusu hii kanuni ya uyeyushaji. Mu + u -> mw haiwezi kuwa ni uyeyushaji kwa sababu hakuna mazingira yanayoruhusu kanuni ya uyeyushaji kutokea.

Mu + alimu -> mwalimu
Mu + ezi -> mwezi
Mu + izi -> mwizi
Mu + okozi -> mwokozi
Mu + umba -> huwezi kupata [mwumba] na mwumba siyo Kiswahili sanifu.

Kanuni ya uyeyushaji hutokea tu pale irabu ya juu (u) inapofuatwa na irabu zingine zenye kimo tofauti; na lengo kuu la mabadiliko haya ni kurahisisha utamkaji kwa kudhibiti kupanda na kushuka kwa ulimi. U inapofuatwa na yenyewe u hakuna sababu yo yote ya kifonetikia kuiyeyusha kwa sababu zote zinatamkiwa mahali pale pale na katika kimo (height) kile kile cha ulimi.

Kanuni za kifonolojia huwa hazitokei tu kiholela bila sababu maalum (mf. mu + uguzi -> mwuguzi). Ukiona mbadilishano kama huu usio na sababu za kifonetiki/kifonolojia basi inabidi uangalie sababu zingine zilizo nje ya Fonetiki na Fonolojia.

Isimu ni sayansi...

(Nilisoma mambo haya kama hobby tu zamani sana ila bado nakumbuka )[/u]
 
Back
Top Bottom