MSAADA WA MACHINE YANGU.


ndammu

ndammu

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2017
Messages
1,017
Points
2,000
ndammu

ndammu

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2017
1,017 2,000
Habari zenu.

Kwa wale wanaoelewa naomba msaada WA utatuzi WA machine yangu ninayofanyia kazi Kwa kujipatia riziki.

Nina machine yangu ya ice cream huu ni karibu mwaka WA nne. Imeanza kuniletea shida lakini mpka sasa bado nahangaika nayo lakini utatuzi WA tatizo bado sijalifahamu.

Leo ni kama siku ya tano compressor inatatizo lá kupata moto sana na kujizima ovyo wakati feni inazunguka huku ice cream ikiyayuka mpka mda mwengine nakosa wateja kwasababu ice cream inayayuka kutokana na compressor haifanyi kazi.

Note: compressor yake ya mwanzo nilibadisha karibu mwezi wa saba huu baada ya kuungua na kuweka nyengine ambayo ndio hiyo iliyonianzia usumbufu toka juzi.

Tatizo hili baada ya kuligundua nilimtafuta fundi baada ya kufika alinambia gesi ni ndogo tuongeze gesi nikatafuta gesi tukaweka baada ya masaa manne Ile hali ilijirudia tena nikampigia simu kumuelewesha na kuniambia atakuja alifika siku ya pili aliicheki na kugundua kuna tundu akaziba tukaweka gesi kwa maranyengine kwakweli hali haikukubali iliendelea tena na leo nilimtafuta kwa simu alifika asubuhi mapema tukaamua tubadili compressor nyengine tulipobadili tukaweka gesi baada ya dakika kama 25 hivi tatizo lá compressor kujizima wenyewe likaendelea kwa mara nyengine.

Kwahiyo kwa mwenye uelewa WA mambo wá tatizo hili naomba sana anifahamishe ili niweze kulitatua.

Kichwa kinaniuma hapa.

Msaada wenu tafadhali na naomba msamaha kwa yule ataekwazika kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,284,750
Members 494,236
Posts 30,838,738
Top