Msaada wa maana ya hii sign kwenye Toyota Runx

La Pronto

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
965
1,142
Habari zenu wadau

Kuna taa imekua ikiwaka kwenye dashboard ya hii gari yangu corola runx na muda mwingine inazima. Nimeuliza kwa baadhi ya mafundi wanasema hizi gari ndo huwa ziko hivyo (inawezekana ndo utaalam wao umeishia hapo). Hivyo nawaomba wadau kama kuna mtu ashawahi kukutana na hii kitu anidadavulie.

Asanteni.

Screenshot_20200514-143158.jpg
 
Mafundi wengi ni wapuuzi wakishindwa kuelewa kitu wanasemaga hio ni kawaida tu kwa aina hii ya gari.

Mkuu ni sign ya tairi moja haina upepo wa kutosha. Hebu shuka nje kagua!

Toyota waliweka sensor maalum TPMS(Tyre.Pressure.Monitoring.System) kwenye baadhi ya gari kama Corrola Axio pamoja na sister car mwenzake Runx / Allex ili kukujuza endapo upepo kwenye matairi umefikia katika critical level.
 
Hyo taa hata mm huwa inawaka hasa gari ikitembea umbali wa km 20 n.k, nilienda mpaka ilala kwa mafundi kujua kwann ile taa inawaka na inaashiria niniii....maana huku mtaan walisema kabisa hawajui ni taa ya nn hasa.

Bac nilipoenda ilala nilikutana na mafundi wa umeme nao ikabidi waingie google ili wajue ile taa ni ya nn hasa, japo walikuta taa inafanana na hyo lakini ilikuwa na tofaut ya ya vimshale vya ndani, yaan ilikuwa haina mishale ya ndani, waliikosa kwenye google japo baadae wakaniambia kuwa ile ta huwa inaendana sana na ABS.

Ikiwa kuna kitu hakifanyi vizur kinachohusiana mfumo wa ABS basi taa hii huwa inawaka na wakati mwingine huwa zina waka zote mbili, niliamini kwa kuwa taa ya ABS ikiwaka na hyo lazima iwake japo kuwa yenyewe inaweza kuwaka bila taa ya ABS kuwaka. Waliishia hapo. Kama kuna mtu anafahamu vema taa hii inaashiria nn bac itakuwa poa kama atatupa elimu.

Hii taa huwaka hata kama matairi yote yana upepo sawa sawa. Nahisi mfumo fulani tu hiv ambao watu wengi hawaujui katika gari hizi.
 
Aisee....nawashukuru sana wadau kwa michango yenu.....hili la kuisha upepo ntaenda nipime tena maana kwa macho tairi zote naona ziko poa....

lakini kuna mdau kaongelea mfumo wa ABS nahisi kwenye gari yangu inawezekana hii ikawa ndio shida coz mfumo wake wa breki huwa naona una mashaka kidogo....
Ntafanyia kazi haya.....nawashkuru sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana ile OBD reader imekosa error kwenye mfumo wa gari yako wakati taa inawaka?
 
Kikawaida tair za mbele huwa inapendeza zaidi ukiweka 35 na matair ya nyuma 40

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kila gari imewekewa kiwango chake cha upepo usijajizie tu kwa mazoea. Ukitaka kufahamu kiwango cha upepo kinachopendekezwa na manufacturer fungua mlango wa mbele (upande wa dereva) wa gari yako angalia upande ule wa lock ya mlango unapofungaga utakuta wamekubandikia kikaratasi kina maelezo mengi pamoja na upepo. Na attach kapicha hapa sijui kama kanaonekana vizuri
Screenshot_20200516-101253~2.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mafundi wengi ni wapuuzi wakishindwa kuelewa kitu wanasemaga hio ni kawaida tu kwa aina hii ya gari.

Mkuu ni sign ya tairi moja haina upepo wa kutosha. Hebu shuka nje kagua!

Toyota waliweka sensor maalum TPMS(Tyre.Pressure.Monitoring.System) kwenye baadhi ya gari kama Corrola Axio pamoja na sister car mwenzake Runx / Allex ili kukujuza endapo upepo kwenye matairi umefikia katika critical level.
Na fielder

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kila gari imewekewa kiwango chake cha upepo usijajizie tu kwa mazoea. Ukitaka kufahamu kiwango cha upepo kinachopendekezwa na manufacturer fungua mlango wa mbele (upande wa dereva) wa gari yako angalia upande ule wa lock ya mlango unapofungaga utakuta wamekubandikia kikaratasi kina maelezo mengi pamoja na upepo. Na attach kapicha hapa sijui kama kanaonekana vizuriView attachment 1451553

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani mbele kwenye uzito mkubwa wa engine uweke 35 halafu nyuma 40? You can't be serious. Mi natumia low profile tyres mbele naweka 45 nyuma 35
 
Back
Top Bottom