Umeme wa 30,000 sio mwingi saaana.
Unaweza ukapiga mahesabu nini kinakula sana kama ifuatavyo.
1. Zima kila kitu.
2. Washa kitu unachotaka kupima.
3. Angalia jinsi ile indiketa la Luku inavyoblink hesabu blinks in 5 min.
4. Zidisha Blinks X 12 kupata blinks in one hour.
5. Kwenye luku imeandikwa blinks ngapi ni unit moja e.g blinks 1000 =1 unit (Sijui actual number sipo karibu na Luku)
6. Blink per hour / 1000 = Units per hour
Hivyo utakuwa umejua kifaa hicho kinakula Unit ngapi kwa saa.
Pia ushauri mwengine ni kuzima vitu kama TV/Radio/DVD player kwenye switch ya ukutani maana hivi vitu vinakula umeme hata kama vipo off.