mungu awatangulie na awatimizie haja ya mioyo yenu.
Lakini.....
Mumejiandaa kulea mwanaaaaaa?...au mnataka mtoto kesho muanze kugombana..karo ya nursery school, matibabu mavazi, shule za academy, vyuo vikuu vya malysia na india etc...mumeyaona haya wakuu au ndio mnataka kutengeneza watoto wanaofuta vioo vya magari kwenye traffic lights.
Tafakarini kisha muchukuwe hatua na mungu awaongoze kwenye tafakuri zenu.
Nenda CCBRT kamuone Dr.Almas atakusaidia,usinywe dawa yeyote kabla haujajua tatizo.
Kutopata mtoto kunasababishwa na mambo mengi,Nendeni hospitali mkapimwe na kama wewe au mkeo hamna tatizo lolote, ni PM nikupatie dawa fulani ya chakula mtakayotumia wote ambayo inachochea uzazi.pole sana kaka inawezekana mara nyingi uapofanya mapenzi, shahawa huwa hiziki sehemu husika kulingana staili unayotumia.. ili yai lilutubishwe linahitaji mbegu wastani wa kijiko cha chakula ambacho huwa na wastani wa mbegu 1000000.
Yaani mwaka 1 unalalamika nina dada mmja alikaa 12yrs bila mtoto na mwaka huu january 2013 kapata mtoto
Mkuu,
Nilishawahi kutoa ushauri kama huu kwa mtu fulani simkumbuki. Basi ngoja nishare na wewe pia nahisi itakusaidia.
Mimi na mke wangu kuna kipindi mwaka jana tulijaribu sana kutafuta mtoto(na yeye ndiye alikuwa na hamu zaidi). Ndugu tulihangaika wapi. Tulitegesha siku zote wapi...... Kwanini hatukuamini(hata mimi sikuamini) kuwa labda tuna matatizo.
1. Mke wangu alishawahi kubeba ujauzito zamani kidogo ila akamiscarry mapema sana. Kwahiyo uwezo wa kushika mimba anao.
2. Mimi pia nilishawahi katika pitapita zangu kujaza wadada fulani hivi so mimi pia uwezo wa kuzalisha ninao.
Tatizo nini??
Stress!!!!! Kufanya mapenzi na kutafuta mtoto kwa stress ndugu haupati kitu!! Yani mtoto anatungwa mwenyewe taratibu bila hata kuwa na mawazo lukuki.
Cha kufanya
Kuna vidonge fulani(ingawa sishauri sana) vya hormones. Nenda pale Kairuki kuna Dr. mmoja mmama hivi(jina nimesahau) ila ukimuulizia utampata. Dr mmama kwa ajili ya kina mama!! Vidonge vyenyewe ni bei ndogo sidhani kama vinazidi Tsh 2000/-
Hii iwe last option ila potezeeni kabisa mambo ya ujauzito. Nyie kuleni raha na tendo la ndoa kwa furaha zote. Badilisheni sehemu, positions ila mkiwa na lengo la kufurahishana. Mawazo ya mtoto weka kapuni.
Amini nakwambia utapewa suprise na utakuja hapa ukiwa na furaha tele.
Je itakuwaje kama hali itaendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao?
Hapo niashauri mkaonane na Daktari bingwa.
Natumai nitakuwa nimekusaidia
Mwenyezimungu mtukutu muumba mbingu na ardhi na vilivyomo duniani amesema hivi:-
"Hakika sisi ndio tunamjalia mtu watoto wa kiume watupu wengine tunawapa wakike watupu wengine tunawachanganyia wakike na wakiume na wengine tunawanyima kabisa na tunampa mtu bila ya hisabu"
Muombe mungu atakujaalia na ujue kua kuna namna ya kuomba ili dua yako ijibiwe jitahidi kula halali na epuka sana haramu
Ukienda CCBRT ULIKOSHAURIWA na KAMA hukuona mafanikio au kama hamjaenda haraka sana kumbilieni MIKOCHENI HOSPITAL KWA SASA KAILUKI hospital mkaonane na DR Clementina ni mtoto wa KAILUKI mwenye hospital ni GYNO Na ni MWISHO wa matatizo ya uzazi.Niamini mimi yule dada amesomea URUSI kwenye mabingwa wa mambo hayo!na anajua sana niamini mimi na hata kama una BIMA YA AFYA AU PRIVATE VYOTE SAWA!UTANIPA JIBU!
Mkuu jenereta, kama walivoshauri wengine, inawezekana bado ni mapema kwa wewe kuwazia sana mtoto kama ndoa yenu ina mwaka mmoja tu....hasa kama tukienda na ile dhana ya kwamba mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu
kwa upande mwingine, una haki kujiuliza labda miezi 12 yote kumetokea nini hadi sasa hamjapata mtoto?
Sina uhakika sana na ufahamu wenu wa elimu ya uzazi, na huenda pia daktari wa CCBRT amewaambia, ila kwenye kupata mimba mambo mengi yanahusika
Nisingeshauri muanze kutumia dawa zozote kabla hamjajiridhisha na hayo hapo juu
- kwanza msiwe na msongo wa mawazo, kwa maana ya stress
- Mfahamu vizuri cycle ya mkeo.....ili mjue ni wakati gani hasa wa kufanya mapenzi..jua ana mzunguko wa siku ngapi, ana enda hedhi siku ngapi, na hivyo unaweza kukadiria kwamba siku ya kuchavusha yai ni siku gani (kama hana tatizo la kiafya na wewe huna pia)
- hakikisheni kwamba kwe mkeo je, hajawahi kutoa mimba, au kuwa na miscarriage, na sababu ilikuwa nini
- Siku hizi kuna 'mlipuko' wa fibroids kwa wanawake wengi, na hii kwa wengine inasababisha wasipate mimba kirahisi
Nawatakia kila la heri
WanaJF, naombeni msaada wenu
Nimeoa mwaka jana, na nampenda sana mke wangu, nampenda sana, lakini toka mwaka jana sijabahatika kupata mtoto, ingawaje kuna siku nilimkuta analia, nikamuuliza unalia nn akasema, ameingia kwenye siku zake while ana hamu ya kupata mtoto, nikamwomba a-calm down though hata mm iliniuma sana.
Hatujaenda bado hosp, lakini naombeni msaada kama kuna watu mna xperience na haya mambo kabla sijaenda hospitali, na tumevizia siku za hatari lakini wapi, please, naombeni msaada wenu wapendwa, natamani sana mtoto.
Asante[/QU