Msaada wa kutoa sumu mwilini na kupungua

Habari zenu ndugu zangu, mimi ni kijana wa umri wa miaka 22 ila na urefu wa 183cm,uzito wangu nin 95KG. Kiukweli na uzito mkubwa kiasi cha kwamba kuna muda nikitembea sana naona shida hasa jua likiwa kali (ingawa ukinitizama kwa kuwa kidogo mrefu utaona kama na mwili wa kawaida ). Ninaonaga matangazo kabla haujaanza kufanya mazoezi unaitajika uondoe sumu kwanza mwilin ili upungue haraka bila hvyo utafanya mazoez na usione chochote.

Sasa naomba njia ya kundoa sumu mwili. Na ninaomba vyakula vizur kwa ajili ya kupungua nilisoma kitabu cha Dr. Berg cha YOUR BODY TYPE moja ya principle anakwambia usile sugar au carbohydrate. Swali langu hapa n moja nitakula nini? Maana kila tunda ninalo liona ni carbohydrate au kuna matunda ambayo siyo carbohydrate? Kwa wataalamu naombeni mpangirio mzur wa chakula ili nione matokeo mapema kwasababu huu mwili naona ubako elekea hypertension inaniita maana naziona dalili kabisa za hypertension.

Asanteni sana kama kuna mtu ana mpangilio mzuri wa chakula labla atataka anicheck basi number yangu ya whatsapp ni 255713696164
Habari
Hapa kwa kweli utapata majibu ya jumlajumla.

Ni kweli kuwa uzito wako ni mkubwa ukilinganisha na urefu wako, kwani kwa urefu wako sitahiki ni kuwa na uzito wa kilo 82 kama kiwango chako cha mwisho.

Ni kweli kwamba vyote vilivyozidi kwenye mwili ni waste/ ziada isiyohitajika.

Ili kupunguza hivyo vilivyo vya ziada ni vyema kujua yafuatayo;

1: Kunatakiwa kupunguza kwa mpangilio vile vilivyozidi.

2: Unatakiwa uchukue kwa mpangilio maalumu kiasi cha viinilishe kwa ajili ya mwili wako bila kuathiri afya yako.

Ili kuyafanya haya vyema:

1: Mwone dietician/mtaalamu wa afya aliyesomea mambo haya. Yeye ataweza kukuelekeza mlo wako uweje kwa siku hii ni kulingana na hitaji la mwili na nini unakifanya kwa siku. Wao wanavyo vipimo vya kila chakula utakachochukua kina uwezo wa kuzalisha nguvu kiasi gani na protini au vitamins. Hakuna chakula usichokihitaji kabisa BALI ni kiasi gani uchukue.

2: Utahitaji kufanya mazoezi LAKINI yasiwe makali sana kwani pia unaweza kuzalisha uchafu mwingi ambao figo zitashindwa kuhimili kutoa nje ya mwili.
Pia mazoezi haya makali yanaweza kuleta shida kwako kama moyo wako utashindwa kuhimili. Mara nyingi hushauriwa mazoezi ya kutembea kwa mwendo wa haraka kidogo kwa dakika 30 mpaka saa moja kwa siku.

3: Ratiba ya mazoezi iwe ni nyepesi na isiyohitaji kutafuta eneo mbali na nyumbani au ofisini. Kwani ni moja ya sababu za kushindwa kuendelea na mazoezi kwa kuwaza lazima niende mapaka kule au lazima nilipe tena au muda hautoshi. Mazoezi huweza kufanyika hata ndani ya nyumba au fensi ya nyumba.

4: Tafakari kuwa hii ni kwaajili ya afya yako kuwa njema, maamuzi yatoke ndani yako na si msukumo toka nje yako.

Nakutakia tafakuri njema na ni jambo jema kwa wazo ulilonalo.
 
Miaka 22 una 95Kg? Aiseeeeee 26 yrs nilikuwa na 57Kg!! Mambo ya kukataza kula ni uzushi cha msingi zingatia unacchoingiza kiwe kidogo kuliko unachotoa!! Fanya mazoezi sana kula kama kawaida!! Kuna watu nawajua wanafukia balaa alafu wembamba tu....Kama ushagundua mwili wako ni wa kufutuka basi jichoshe sana,usikae kizembe zembe.
Mimi nilikuwa nanepa ilihali ninafanya mazoezi
 
Acha kunywa sukari kwenye chai kwa muda wa miezi mitatu uone utakavyopungua huku vyakula vingine unakula Kama kawaida, baada ya miezi mitatu uwe unatumia asali Kama mbadala wa sukari na ukikosa asali uwe unatumia sukari nyeupe ile wanatumia watu weupe na soda unakunywa kwenye occasion au ukisikia kiu ya sukari unalamba glucose.
 
Back
Top Bottom