Nisaidie modal ya kulipwa mkuu Luse
Ooh, sorry nilikuwa sijaiona hii.
Nimefatilia link kwa hiyo natakiwa kulipia domain 25,000 hafu pesa ya kudesign website ambayo ni makubaliano na designer ntakayefanya naye kazi, sasa kwa ushauri wako bila matangazo yoyote kwa watu kuingia na kusoma inalipa au mpaka upate mtu wa kutangaza kwenye page yako?
Ndio tsh 25,000/= ya domain na usisahau kuna seperate pricing kwa ajili ya hosting. Bei yake huwa inatofautiana kutoka kampuni moja na nyingine.
Kwakuanzia, sio lazima utafute designer kwaajili ya kudesign website yako, zipo free templates/themes mbalimbali unaweza ukazitumia au zingine ni za kulipia ila hazina bei sana. Tena mara nyingi webdesigners wa bongo ndo huwa wanafanya hivyo, with the exception ya wachache. Unakuta amepewa kazi ya kudesign a website anaenda kutafuta a free template/theme au ananunua template halafu anaipachika kwenye website yako. Sana sana ataimodify hiyo template kidogo tu. Mwishowe unakuta website yako haistand out kivile au mko wengi ambao website zenu zinaelekeana.
Sasa si bora mtu ununue mwenyewe template na kui-install, kuliko kumlipa a web designer ela kubwa halafu akadeliver kitu ambacho hakina tofauti na kufanya mwenyewe. So keep that in mind kabla hujampa kazi yako web designer yoyote yule.
Tuje, kwenye swali lako kuhusu modes za kulipwa.Kuna njia nyingi za kulipwa kupitia a website/blog, both directly and indirectly.
Tuanze na indirectly kwanza.
Lets say labda wewe ni daktari wa magonjwa ya kina mama, na una clinic yako ambapo watu wanaweza wakaenda kuhudumiwa na kusaidiwa matatizo yao.
Kwahiyo unaanzisha a website ya clinic yako na unakuwa unaandika articles labda twice a week zinazohusiana na mambo ya health ya kinamama. Pia unaprovide contact information incase mtu atahitaji kukutafuta na kupata ushauri.
Kwahiyo mtu akienda online na akigoogle, kuhusu issue fulani, anaweza akakutana na moja ya article zako, na article zako ukiziandika in an informative way na kuonyesha credibility, ni rahisi mtu kuchukua contact information na kuamua kukutafuta, ili umsaidie na tatizo ambalo anaweza kuwa nalo.
Hii inamaana unatumia blog kama njia ya kujimarket. Inaitwa "content marketing". So kama unavoona unaweza usilipwe moja kwa moja kupitia blog yako, labda kwa kuweka matangazo etc. Lakini hiyo blog inaweza ikawa inakuletea wateja na watu watakao lipia service zako, through wao kusoma mada zako na kukutafuta offline ili uwatatulie shida zao.
Tuje sasa kwenye jinsi unavoweza kulipwa kupitia blog yako directly.
First ni kwakuweka matangazo.
Kuna two main ways ya kuweka matangazo kwenye blog yako.
Ya kwanza ni kwakujiunga na ad network, na moja ya ad network maarufu ni google adsense. Hii inamaana hiyo ad network anakuwa kama middle man, yani advertiser anailipa the ad network halafu hiyo ad network inadisplay tangazo la huyo advertiser kwenye blog yako. So kwenye kukulipa, the ad network inachukua percent fulani ya malipo. Moja ya faida kuu ya kujiunga na ad network hi kuwa huhitaji kuangaika kutafuta watu ili watangaze kwenye blog yako.
Njia ya pili ya kutangaza kwenye blog yako ni kwa kumuondoa the middle man, yani ad network, na watangazaji kukulipa wewe moja kwa moja. Hii inamaana unawatafuta watangazaji mwenyewe ili watangaze kwenye blog yako, au kama blog yako ni famous, watangazaji wenyewe watakuwa wanakutafuta. Kama unaviewers wengi ni rahisi kupata income ya kutosha kupitia hii njia.
Sema njia ya kuweka matangazo kwenye blog, huwa inategemea sana kulingana na idadi ya watu wanaotembela blog yako.Kama watu niwachache, usitegemee kupata ela nyingi.
Njia ya pili yakulipwa directly kupitia blog yako, ni kwakuoffer courses.
Tuseme labda unablog kuhusu mambo ya kilimo. Na unakuwa unaandika mada mbalimbali ambazo ni very informative kuhusu kilimo. Na watu wanazipenda. Sasa kulingana na feedback ya wasomaji wako na maswali ambayo unakuwa unaulizwa mara kwa mara, unagundua kuwa watu wangependa kujua zaidi labda kuhusu ufugaji wa kuku. So unachofanya ni unaandika kitabu kinachoelezea kwa kina kuhusu ufugaji wa kuku, changamoto zake na jinsi ya kufanikiwa katika biashara hiyo. Hiki kitabu kinakuwa katika digital format e.g pdf. Halafu unakiuza kwa wasomaji wako. Inamaana mtu akikulipa, anapata link ya kitabu hiki ili, aweze kukidownload.
Mfano mwingine, tuseme wasomaji wako wangependa kujua jinsi ya kulima uyoga. Kuanzia mwanzo kabisa mpaka kuvuna. Unaweza ukatengeneza course, yenye video, picha, audio na makala mbalimbali ambazo zinaelezea kuhusu ulimaji wa uyoga. Kisha hiyo course unaiweka katika section ya blog yako ambapo mtu hawezi kuiaccess mpaka alipie. So mtu akilipa ndo anapata labda username na password ili aweze kuaccess hiyo course.
Hii njia ya kuuza vitabu au course kwenye blog yako huwa haitegemei watu wangapi wanatembelea blog yako.
Tofauti na kuweka matangazo kwenye blog ambapo ukiwa na viewers wengi ndo ela inakuwa kubwa. Ila njia ya kuuza vitabu au course kwenye blog, hata kama unawatu wachache, bado unaweza ukapata ela nzuri tu. As long as umetengeza kitu ambacho watu wanakihitaji na wako willing kukilipia.
Mfano tuseme umeandika kuhusu kitabu cha kufuga kuku na unakiuza kwa elfu 20 tu. Then tuseme huna viewers wengi wanaotembelea blog yako regularly, labda kwa mwezi hawafiki hata watu 1000. Ila kati ya hao watu elfu, watu 20 wakaamua kununua kitabu chako. That means umetengeneza laki mbili.
Ila tukitumia namba hizo hizo za tuseme watu elfu wanatembelea blog yako kwa mwezi, halafu ukataka kuweka matangazo. Sahau kabisa kumpata mtu atakaekubali kutangaza na wewe. Na hata akikubali usitegemee kupata ela nyingi, usishangae mtu labda akakwambia atalipa elfu 20 tu, kwa mwezi au hata kidogo zaidi.
Anyways hizo ndo njia mbalimbali unazoweza kulipwa ukiwa na website/blog. Hopefully nimeelezea vizuri na utakuwa umepata kitu.