Mkuu, marekebisho kidogo kwenye kunukuu. Kwenye capital namaanisha kuanzia 70,000/=. ila sidhani kama inaweza kuzidi more than 150,000/=, ingawa kuna host wengine wanacharge much higher. Hapa namaanisha hosting na kununua domain.
Na my suggestion ya kuhusu kuanzia na a whatsapp group kwanza, my main point ni kuhusu proof of concept. Yani you starrt with something small kwanza, halafu ukiona inagain traction ndo una expand to kutengeza website and so on.
Ila kama unataka kuanza na route ya kutengeneza website. Here are the estimates.
Kununua domain, inayoishia na .com hii huwa inacost dollar 10 na unalipia kwa mwaka. A good place ya kununua hii ni this website:
Domain Names - Cheap Domain Names | Namecheap.Com
Ila kama utataka kununua a domain name inayoishia na .tz e.g .co.tz, itabidi utumie kampuni ya kibongo kuregister. Hii inacost tsh 25,000/= na unakuwa unalipia kwa mwaka pia. A good place yakuanzia ni hapa:
tzNIC | Tanzania Network Information Centre - .tz registry | .tz domain names , hii ni a partial government agency inayohusika na registration ya .tz domain, You don't register your domain name with them, ila hawa ndo wanatoa accreditaion kwa makampuni ya kibongo ili waweze kuregister .tz domain. Hii hapa ni link ya their accredited registers:
tzNIC | Tanzania Network Information Centre - List of registrars
Sehemu unayonunua a domain , sio lazima uhost website yako pia hapo hapo. This means unaweza ukanunua domain name yako bongo halafu website ukaihost nje ya nchi au ukanunua domain nje ya nchi halafu website ukaihost bongo. Au unaweza ukanunua domain kwenye kampuni moja na kuhost website kwenye kampuni nyingine.
Kuhusu kulipia a webhost, hapa ndo inategemea, kuna wengine unaweza ukalipa per month, per 3 months, per 6 months na per year. Ila the most popular option huwa ni kulipia per year. Na good webhosts wa nje unaoweza ukawatumia ni,
Web Hosting Crafted For Top Website Performance & Speed na
Website Hosting | Shared Web Hosting With cPanel - Bluehost . Hizo link zinaenda straight to the pricing page, so unaweza ukafanya comparison.
Ukitaka uhost website yako bongo, hapo sina experience kuhusu hicho kitu. ila unaweza ukauliza kule jukwaa la tech kuwa yupi ni webhost mzuri kwa bongo. Wanaweza wakakupa mwangaza.
Tuje sasa kwenye kumake your website look good. Kuna 3 options, unaweza ukatafuta free themes kisha ukainstall kwenye blog yako, au ukanunua themes mwenyewe, huwa zina cost kuanzia dollar 39 upto $199 , kulingana na theme utakayoitaka. The third option ni kumtafuta mtu akadesign your website. Hii huwa ndo the most expensive option, na inacost si chini ya tsh 300,000/= kwa designers wa bongo. Sema ishu inakuja kwenye kumpata web designer mzuri.