Msaada wa kununua gari

Msaada wa kununua gari

Nina sh 6000000 nataka kununua gari ni gari gani nzuri kwa maana ya ulaji wa mafuta, inayoweza kustahimili maeneo mbalimbali ya tanzania naomba ushauri wenu wana jf sio muanze kunitukana maana siku hizjf mmm!

Hapo unaongelea gali kama FAN CARGO, SUZUKI MARUTI, DUET, SUZUKI JIMMY, STARLET, TOYOTA VITZ, TOYOTA ist and the like. Kila la kheri mkuu!
 
Mkuu ingekuwa rahisi kama ulivyoandika hapa kila mtu hapa mjini angesukuma ndinga. Aliyekuambia mtumishi wa serikali halipi ushuru ni nani?

Bora umesema wewe, kila nikisoma anavyosisitiza eti mtumishi wa serikali halipi ushuru nabaki kuguna tu.
 
Mmh mtumishi wa serikal halip ushuru? Mkuu hebu toa ufafanuz zaid

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Chukua starlet mzee. Sababu za msingi 1. It can accomodate your cash 2. Durable 3. Economy 4. Easy to run. Kwa pesa uliyonayo utapata starlet mpya I.e used japanese, ukiforce kununua gari kubwa zaidi utajikuta unachukua gari used tanzanian. Na ukishanunua tu gari kwa mtu I.e wa hapa tz, ujue utakua best frend wa mafundi wote. Huo ni ushauri wangu tuu kk

Hahaaaaaa kweli mkuu
 
Siyo Funcargo
Inaitwa Gurumo

Yaani nimecheka sana hapa hd kifua kimenikauka kwa kicheko,maana njna mtani wangu ana funcargo,baada ya kusoma hapa nikampigia simu kumwambia kuwa siku hizi funcargo zinaitwa GURUMO,amekasirika kasema atauza haitaki tena ndio hapa sina mbavu mkuu.
 
Kwa pesa ulokuwa nayo utapata gari ndogo sana akina vitz na stalet,lkn umesema inayohimili mikiki kidogo,hapo lazima uongeze peaa kidogo alau upate carina TI,kinyume na hapo sina ushauri
 
Njoo nikuuzie Nadia ila ongeza hela kidogo
 
päiva;8214164 said:
Bora umesema wewe, kila nikisoma anavyosisitiza eti mtumishi wa serikali halipi ushuru nabaki kuguna tu.

Mmh mtumishi wa serikal halip ushuru? Mkuu hebu toa ufafanuz zaid

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Hao Ndo ccm wakwepa ushuru labda ndugu ya lukosi angesema wanapunguzo la asilimia fulani Lakini sio kwamba hawalipi ushuru
 
Kama huyo ni mfanyakazi wa serikalini hiyo hela ni nyingio sana kwani atapata kitu swafi kwa bei nafuu
Nissan xtrail ya 2004 unapata kwa £1,200 na freight ni £800 jumla ni £2000 sawa na 5m zilizobaki analipia port charges gari iko nje ,

MTUMISHI WA SERIKALI HALIPI USHURU
Wewe huijui Tanzania inavyoendeshwa, unadanganywa na nani kuwa mtumishi wa serikali halipi kodi?
 
Hatuwezi jua sana maana hatuko moyoni mwako ila mara nyingi hata wanaouza kwa sababu gari ina matayizo wanasema ili wanunue......... Kwa ajili ya familia. Mshauriwa kuwa makini
 
Kama huyo ni mfanyakazi wa serikalini hiyo hela ni nyingio sana kwani atapata kitu swafi kwa bei nafuu
Nissan xtrail ya 2004 unapata kwa £1,200 na freight ni £800 jumla ni £2000 sawa na 5m zilizobaki analipia port charges gari iko nje ,

MTUMISHI WA SERIKALI HALIPI USHURU

Kweli mkuu? Hazisumbui zikija bongo hizo gari za UK? Nipe details nijitose mkuu wangu.
 
Wana JF, msiangalie bei ya gari tu.. Kumiliki gari ni jambo moja, tena jepesi tu. Lakini kutunza gari ni jambo jingine gumu, linahitaji uwezo wa kutosha na nidhamu ya matumizi.. Gari lenye cc ndogo, 650 mpaka 1500, SUV, itakufaa. Kuna gharama za kila siku, mafuta, kila mwaka, bima, leseni ya TRA, muda maalumu, service kila baada ya km 3000, vipuri, tairi nk..
 
Njo nikuuzie corona premio INA speed 260 ,haili mafuta ,kwa mwendo kiboko ,mm nicngeuza lkn nahiyaji kununua Prado kwa ajili ya familia

mambo ya kizamani sana haya, eti ina speed 260 hahahaaa!
 
Kama huyo ni mfanyakazi wa serikalini hiyo hela ni nyingio sana kwani atapata kitu swafi kwa bei nafuu
Nissan xtrail ya 2004 unapata kwa £1,200 na freight ni £800 jumla ni £2000 sawa na 5m zilizobaki analipia port charges gari iko nje ,

MTUMISHI WA SERIKALI HALIPI USHURU

Mkuu ingekuwa rahisi kama ulivyoandika hapa kila mtu hapa mjini angesukuma ndinga. Aliyekuambia mtumishi wa serikali halipi ushuru ni nani?

Afadhali wana CCM msaidiane, angesema mwingine ungesikia siasa zishaanza kuingizwa.

Kwa kifupi ni kweli kwamba si kodi zote huwa exempted, nafikiri ni import duty huwa wanatoa lakini kuna VAT 18% lazima ulipe.

Hata hiyo gari uwe umepewa bure, custom value ya X-trail ya 2004 ni USD 4,980 kwa hiyo hata kama ni VAT peke yake utatakiwa kulipa then utalipa kodi, at minimum USD 896 or TZS 1.47m
 
Back
Top Bottom