Msaada wa kufunga ndoa

Hiyo harusi itengee kama 8m kisha nenda kunduchi beach hotel weka order ya BUFFEE kwa idadi hiyo ya watu wako.

Ongeza na vinywaji vikali ,zungumza na live band inayopiga pale, weka mambo sawa tena yawezekana mkafurahi saana na kuwa bonge ya sherehe inayojiendesha yenyewe kama mamtoni.

Ikiwezekana Hata Padre/mchungaji/shekhe/DC mkamwita pale kwa mpangilio maalum shughuli ikafanyika Poa kabisa.
 

Msosi sahani 100 @ 12,000 = 1,200,000/-
Vinywaji 100 @ 2500 = 250,000/-
Ukumbi + mapambo + Mc = 400,000/-
Chumba cha hoteli = 150,000/-
JUMLA............................... Tzs 2,000,000

Hapo msosi sio tenda ni hotelini hapohapo. Vinywaji utabalance kulingana na mahitaji.
 
Amekua mtu wa kununa nuna muda wote
Ukiwa muongo, usiwe msahaulifu ...mbaf.. kabisa...[emoji34] [emoji34]
 
Kuhusu kumbe mkuu niliwaza uwe wa laki tano na hii harusi itafanyika mkoa wa ruvuma ,,,,,haya mkuu naomba mchanganuo wako sasa ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mkuu kwa bajeti hiyo mbali sana na hii sherehe ni mkoa wa ruvuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimeupenda mchanganuo wako yaani sana nashukuruuuu kama una lingine unaweza pia kunishaurii

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umetisha
 
buget yako ndo itakuguide
location
vinywaji utakavyovitaka
vyakula utakavyotaka
decoration
Mc unayemtaka
kaka unatokea mkoa gani coz kama ni northern zone jiandae kulaumiwa bora uifanyie mjini
 
Yaan nn utuzalau hutaki tuchange?? Kwaiyo umeamua kuita watu wachache tusile ubwabwa??

Acha uchoyo tuna pesa zetu hiyo hali unayoisema tz sisi haituhusu tutakuja na mbege zetu

unalinga wewe mtoto wa massawe hii haikubaliki

ahaaa mkuu natania nawaza kama unatokea huku kwetu kolomije inavyokuwa. Watu wana mind sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…