Msaada wa kuandika madai ya BIMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kuandika madai ya BIMA

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mtambuzi, Apr 12, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wakuu heshima kwenu.
  Ninaomba mwenye utaalamu wa kuandika madai ya Bima anisaidie. Nilipata ajali ya kugongwa na gari Octoba mwaka jana na hatua zote za kipolisi zimetimia. mpaka sasa bado kesi haijaenda mahakamani baada ya dereva kukimbia. hivyo nimepewa nakala zote za shauri hilo na Polisi makao makuu ambazo zinaniwezesha kuanza mchakato wa madai yangu ya Bima. lakini tatizo nililo nalo ni kwamba sina utaalamu wa kundika madai hayo.
  Nilivunjika mkono wa kulia karibu na kiganja.

  Habari ya ajali yangu iliwahi kuandika hapa na memba mwenzangu kwa kuisoma waweza kubofya hapa:

  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/185673-mzee-mtambuzi-wa-jf-amepata-ajali-asubuhi-hii.html

  Natarajia kupata msaada wenu.

  pamoja Daima
   
 2. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kuanzia tu ni lazima uwe unajua mpaka sasa umetumia kiasi gani nikimaanisha uwe na ushahidi wa gharama zote tangu ulipogongwa eneo la ajari hadi matibabu yake. Ukishaweka sawa vitu hivyo ni lazima ujue hiyo daladala bima yake ni ya kampuni gani ili uweze kwenda kudai fidia ya hasara uliyoipata. Hata kama dereva wa gari alikimbia ninaamini kuwa hiyo gari inajulikana ni ya nani kwa hiyo hapo sioni ni kwa nini kesi haijaenda mahakamani kwani mmiliki wa gari ni lazima awajibike pia. Anyway cha msingi ni kwenda kampuni aliyokatia bima na kisha utapewa form ya madai ili uweze kufuatilia malipo yako.
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Gharama zote za matibabu zimelipwa na mwajiri wangu. Kwa hiyo ina maana hakuna nitakacholipwa?
   
 4. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  polee sana ndugu ila ninavyojua hauwezi kushinda kesi ya bima mpaka yule dereva aliyekugonga apatwe na kosa la jinai, therefore among the requirement to win insurance case is through production of judgment which hold the driver liable for criminal offence connecting with ur case, ukikutana na advocate anayejua mambo ya insurance vizuri atakupiga preliminary objection na mchezo unaishia hapo
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ndio imekula kwangu?
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Anza na kutambua uhalali wa gari iliyokugonga, Kama mamba iko sahihi hatua ya pili nenda kwenye regulatory authority ya bima kwani kila gari lazima iwe na cover at least third party, hapo Utajua owner wa gari na insurer. Ukiwajua hao unalala nao mbele, in case of third party insurance nakala ya traffic case sio muhimu, cha muhimu ni kuwa, at the time of the accident the insurance was valid. Kazi itakayobaki ni kuthibitisha negligence au recklessness.
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu, document zote ninazo na hata owner wa gari nimeshaonana naye tatizo tu ni derevaambaye amekimbia na mmiliki wa kampuni ya Bima niliwahi kuonana naye kwenye function fulani na nilipomueleza alinipa business card yake na kunishauri niandike claim ya madai nikieleza kwa nini nataka nilipwe then ataangalia kama madai yangu yana mashiko. alinitahadharisha kwamba si lazima nikipata ajali nilipwe hiyo itategemea na athari niliyoipata kama ina mashiko then watalipa.

  Tatizo langu mimi sio mtaalamu wa kuandika madai ya Bima ninachohitaji ni muongozo.
   
 8. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Pole mkuu......nadhani ukianzia IFM pale wana walimu wanafundisha hii kozi ya Insurance na consultancy ni sehemu ya kazi ya mwana taaluma yoyote. Ni matumaini yangu kuwa ufumbuzi wa kitaalamu waweza kupatikana kuanzia pale. Na yawezekana humu pia tunaweza kupata links zao au wao wenyewe

  Wish you all the best
   
 9. n

  ngilenengo1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 933
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Fanya yafuatayo:
  1. Hakikisha unayo "Insurance Cover note" ya Gari iliyokugonga
  2. Nenda na hiyo cover note kwa Bima ya Gari iliyokugomga, waambie unataka wakupatie " Claim Form"
  3. Jaza Claim form yako na uweke viambatanisho vyako vyote vya madai unayotaka wakulipe.
  4. Baada ya kujaza Claim Form irejeshe kwenye kampuni ya Bima ulikoichukulia.
  5. Waombe wakupatie Claim number ya fail lako.
  6. Waulize kama kuna uthibitisho/maelezo mengine yoyote wayohitaji
  7. Waombe wakupatie contact person utakaekuwa unawasiliana nae.
  8 Endelea kuatilia majibu yako

  Wasalaam,
   
Loading...