awamuyetu
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 329
- 166
Habari za asubuhi ndugu zangu wanajukwaa, mwenzenu niliingia mjini macho juu nikapigwa, niliuziwa simu chini ya mnara kama wajanja wa zamani walivyoita. Niliuziwa simu barabarani ilikuwa inafanya kazi vizuri tu, nilitumia kwa muda mfupi kama miezi miwili baadaye nikaihifadhi baada ya kupata simu nyingine. Majuzi nimeiwasha ili nimpatie mtu line zote zimegoma kusoma mtandao japo handset yenyewe inatambua line iliyowekwa ni ya mtandao fulani ila network ndo haikamati. Kama kuna wajuzi wa mambo naomba msaada wa ku bypass TCRA.