Msaada wa Kisheria

Mkulima

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
1,034
1,022
Wakuu,

Kampuni yangu ina ugomvi na serikali ya mamlaka ya mji mdogo kwenye moja ya wilaya zetu. Juhudi za kutumia njia za kawaida kutatua tatizo zimeshindikana. Wanagoma kutoa leseni ya biashara kwasababu za kipuuzi mno. Naamini walikuwa wanataka rushwa kwa kujifanya kuchelewesha mambo na kuja na madai ya ajabu ajabu. Mimi nimeweka msimamo wazi, sitoi na wala sitatoa, bora hata waninyime kabisa hiyo leseni.

Je unaweza kuwapeleka hawa watu mahakamani? Hapo unawashitaki mamlaka ya mji mdogo au unaishitaki halmashauri ya wilaya.

Pia kesi kama hiyo unaifungua kwenye mahakama gani? Kama imeshindikana kupata haki kwenye vikao vya watendaji basi tuende hata mahakamani.

Nitashukuru kwa mabingwa wa sheria kunipatia elimu tosha. Hapa au kwa PM kote sawa tu.
 
Una haki yako na unaweza kuwashitaki na kuwalazimisha kukupa leseni kama umekidhi vigezo. tafuta mawakili katika eneo ulipo na watakupa msaada wa ziada.
 
Kwa suala la rushwa ni vizuri kuwashirikisha TAKUKURU ili kuangalia kama wahusika wanaweza kutiwa adabu.

Kama TAKUKURU hawatakuwa na msaada basi mahakama yenye uwezo wa kuangalia kama vyombo vya utawala vya serikali vimefuata sheria na kama vimetenda haki katika kutekeleza majukumu yao, na kutoa amri ni Mahakama Kuu pekee.
 
Back
Top Bottom