Msaada wa Kisheria

Lamisa Danish

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
285
626
Wakuu habari zenu!

Katika pitapita zangu za kula maisha na ujana weekend iliyopita nikajikuta niko Mwanza kwenda kuangalia mpira Simba na Ruvu Shooting aka Barcelona ya Bongo wazee wa pira mpapaso.

Weekend ilikuwa traaamu hatari mana hali ya hewa ilikuwa murua kabisa mvua kama inataka kunyesha ila hainyeshi,yaan wingu linakuja halafu linapotea ili mradi raha na burdani kwa sisi watumiaji wa maji ya dhahabu.

Basi bhana hapa na pale nikapata rafiki mwenyeji mwenyeji uwanjani pale CCM Kirumba ambae nae amekuja kutazama mpira wa Simba ingawa nae shabiki kindaki kindaki wa Dar Young Africa kama ilivyo kwangu pia.

Tukatazama mpira ukaisha tukaanza kupitia maeneo mbalimbali ya kinywaji ili kupoza makoo na kufanya utalii wa ndani,basi bhana tukaanzia Villa park tukaja Weekend car wash tukaenda Maseti, Plazma then kwenye SAA kumi alfajiri nikarudi hotelini kwangu nilikofikia Hotel Kingdom.

Huyu mwenyeji wangu,rafiki yangu na shabiki mwenzangu wa mitaa ya twiga na jangwani ni MTU mcheshi,mkarimu,mpole na anaependa kampani. Kiukweli nilienjoy sana kwa kampani yake. Sikutarajia kupata rafiki honest, humble na gentleman kama huyu.

To make long story short, ktk mazungumzo yetu ya kubadilishana mawazo ya hapa na pale huyu bwana ni Muajiriwa wa kampuni fulani iliyoko hapa Daslam ambapo ni makao makuu ila yeye yuko kule Mwanza iliko ofisi yao ndogo, branch.

Alihamishwa miaka sita iliyopita,lakini ktk uhamisho huo kukiwa na makubaliano ya kukaa mwaka mmoja tu then atarudishwa tena makao makuu ila katikakipindi chote hicho amekuwa akipigwa danadana kila anapoulizia suala la kurudishwa tena huku hadi sasa ambapo ana miaka sita sasa.

Mke na familia aliicha huku Dar,kwa kudhani baada ya mwaka mmoja angerudi tena kuungana nao ila imekuwa kinyume chake.

Baada ya kuona hakuna matumaini yeyote ya kurudishwa akaona heri afanye uamuzi achukue familia akae nayo Mwanza ili ahamishie maisha huko sababu suala la kurudi tena Dar limekuwa gumu.

Chakushangaza boss wake hataki kumpa pesa ya kulipia pango la nyumba kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake.yeye anaishi kwenye self yenye chumba kimoja kisichotosha kuishi na familia yote endapo akiihamisha Mwanza.

The Guy anadai hapa Daslam ana nyumba yake ambapo ndipo familia yake ilipo kwa maana ya mke,watoto nk.sasa yuko njia panda asijue cha kufanya.Kazi anaitaka popote atakapo pangiwa ila kwa kufuata taratibu za kazi.

Mana amechoshwa kuishi bila familia hiyo moja,Pili akibeba familia gharama za pango LA nyumba itabidi abebe yeye ilihali makubaliano hayakuwa hayo boss amemgeuka akiwa site na hataki kusikia suala lolote LA kutoa pesa ya nyumba ya kuishi.

Je Sheria,kanuni na taratibu za kazi zinasemaje kuhusu situation kama hii ya boss kugoma kulipia sehemu ya kuishi ya mfanyakazi na kwenda kinyume na makubaliano yenu?

The Guy anafikiri kurudi eneo LAke LA kazi alipoajiriwa mwanzo by force,Je inaweza kuleta shida gani za kisheria zitakazo sababisha akose haki zake za msingi iwapo boss atareact kwa uamuzi wake huo?

Nataka kumsaidia rafiki huyu mwema apate msaada,nimejaribu kueleza kifupi yale ninayoyakumbuka kama kutakuwa na maswali mengine ya kujazia ili nielekweke nitayajibu chini.

Asante.
 
Walisaini Mkataba?

Kama ndivyo Kuna hiko kipengere cha kumlipia kodi ya nyumba mtumishi? Tuanzie hapo kwanza
Mkataba alionao ni ule wa ajira tu ila huo unaosema wa kulipiwa kodi hakuna,sababu kituo chake cha kazi ni Dar huko Mwanza walifanya makubaliano ya mdomo tu ambayo boss wake ameyakiuka baada ya kumuhamisha kituo kingine cha kazi.
 
Madai yasokuwa na maandishi ni magumu lakini pia kubishana sana sio ishu kama anachukua familia anaweza tafta nyumba ya kujitegemea
 
Yawezekana pia alihamishwa kimkakati ili boss afaidi tunda la mke wa jamaa na hataki familia imfuate jamaa aliko. Dunia uwanja wa fujo.
 
Back
Top Bottom