Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini(labour law) sheria namba 06 ya mwaka 2004 ni wajibu wa mgonjwa au ndugu/mtu wa karibu wa mfanyakazi ambaye ni mgonjwa kutoa taarifa za kutokuhudhuria kazini kwa mfanyakazi kwa sababu ya ugonjwa,haijalishi wakati unatoa taarifa lazima uwe na ripoti ya hospitali kama daktari bado hajathibitisha nini hasa tatizo lake,ispokuwa baadaye ndipo mfanyakazi huyo atalazimika kupeleka vyeti vya hospitali au kituo cha matibabu kuthibitisha kuwa alikuwa mgonjwa na akapata tiba.Na mgonjwa huyo halazimishwi kwa mujibu wa sheria za kazi kwenda kazini akiwa mgonjwa na wala hatokuwa mtoro kisheria kwa kuwa sheria imeweka wazi kuhusiana na haki za mfanyakazi ikiwemo haki ya likizo ya ugonjwa(sick leave) rejea kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira Na Uhusiano Kazini