As Salafiyyu91
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 2,537
- 2,530
Ndugu wanajamvi kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba tuungane kusoma yanayowasibu ndugu zetu
Kuna familia moja ambayo mpaka sasa ina watoto 6 wengine wameshatangulia mbele za haki ambao wamezaliwa na baba mmoja lakin wanne kati yao wamezaliwa na Baba mmoja na Mama mmoja,
alafu mtoto mwingine kazaliwa na Baba mmoja pamoja na wale wanne lakini kwa mke mwingine ,
Alafu wa mwisho ni mtoto wa kiume ambaye kazaliwa nje ya ndoa huyo ndio sababu ya kuandika Uzi huu
Kimsingi huyu mtoto wa mwisho 6 ambaye kazaliwa nche ya ndoa amekuwa Msumbufu, Mgomvi na akiwaonea watoto halali wa familia ya Mzee Saidi kisa eti ni watoto wa kike.
Ndugu hawa wameachiwa Nyumba moja kubwa na ina uwanja mkubwa lakin kwa sababu wao wamekuwa ni watoto wa kike basi huyo mdogo wao wa njee ya ndoa amekuwa akiwapelekesha anavyotaka yeye.
Imefikia stage wamepangisha mpangaji katoa hela ya pango kisha wakagawana pamoja na huyo mtoto wa njee ya ndoa lakin yeye ameamua kumleta mpangaji mwingine nakumpangisha bila ya kuwa shirikisha wenzie jambo ambalo limeleta mgogoro mkubwa kiasi kwamba mpangaji wa mwanzo anataka arudishiwe kodi aliyoitoa.
Sasa hawa ndugu wa 5 kodi wamesha gawana na wameila, alafu sasa hivi mpangaji wa awali amekuja juu anataka pesa zake arejeshewe kwaiyo kumetokea mgogoro mkubwa mpaka sasa haujatatulika
Ndugu hawa 5 wameona sasa bora wauze nyumba yao hiyo ili wagawane hela mambo yaishe lakin cha ajabu huyu mtoto wa nje ya ndoa hataki nyumba hiyo iuzwe anataka aendelee kuitawala atakavyo kisa warithi hao ni watoto wa kike ya yeye ni mwanaume
Je ndugu wanajamvi hawa watoto halali wa mzee said ambao wapo 5 wafanye nini iliwapate haki yao
Nawasilisha....!!!!