Msaada wa kisheria unahitajika haraka

Nyrum

Senior Member
Aug 11, 2013
124
41
Habari wanajamvi, nimekuja huku leo ninahtaj msaada wenu. Japo sio mwandishi mzuri lakin naamin mtanielewa.

Mimi ni msichana niliolewa na nikabahatika kuzaa watoto wawili (mapacha) wa kike na wa kiume. Watoto wangu wana umri wa miaka2 na miez6.

Kulitokea ugomvi upande wa ndugu zake hasa mama yake na wajomba zake ndipo wakamwambia mtoto wao anipe talaka aniache. tulifunga ndoa ya kiislam ambayo ndugu zake hawakuridhia,

sasa kilichonifanxa nije kwenu leo ni kwmba mwanaume yule hawahudumii watoto ipasavyo ikiwa ni pamoja na kodi ya nyumba wanayoish wanawe, chakula, matibabu, mavazi. yeye anatoa elf80 kila mwez eti ndo huduma ya watoto tena wawili.

akishatoa hyo pesa bas hajui kununua nguo ya mtoto wala panadol wakiumwa. mimi ni mwanafunz wa chuo, watoto wangu wanaish na mama yangu mzazi. lakin inafkia kipind mama anakosa hata kodi ya kulipa. nawalea watoto katika mazingra magumu wakt baba yao yupo na pesa anazo.

nahtaj mchango wenu ndugu zangu, ushauri na maelekezo nifanyeje ili wanangu wapate haki zao za msingi? Kumbuka wao hawahusiki na kuachana kwetu. tafadhali ndug zangu. kwa mwenye nia ya kunisaidia aniPM au anicheck kwenye 0782701288.

ahsanteni!!!
 
hebu jaribu kwenda ofisi za ustawi wa jamii walau ukapate muongozo
 
Hebu karibu kwenye firm yetu tutakusaidia...0758144803 tupo posta..
 
Binti mimi nakushauri nenda Tawla kama usipo waelewa nenda ustawi wa jamii..utasaidiwa tuu wala usiwaze sana..
 
ukibonyeza hapo tunatoa msaada wa kisheria pia ,bure. bofya SHERIA KWA KISWAHILI
 
Back
Top Bottom