Msaada wa kisheria tafadhari!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria tafadhari!!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Sebali, Oct 18, 2011.

 1. S

  Sebali Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtumishi wa sekaliri, nipo masomoni kwa sasa lakini mara tu baada ya kuanza masomo yangu nilikatiwa mshahara lakini nashanga 'salary slip' zinaendelea kutoka huku mshahara nikiwa sipati. Walinikatia huo mshahara baada ya mimi kwenda masomoni huku nikiwa sina barua ya ruhusa ingawa nilikuwa na sifa ya kupata ruhusa. Je hizi fedha zangu zinaenda wapi wakati zinatoka kila mwezi huku mimi nikiishia kupata salary slip ambapo pesa haiingizwi kwenye akaunti yangu? Je ninauwezo wa kupata pesa yangu yote pindi nikimaliza masomo yangu na kurudi kazini kwa vile kwasasa namalizia mwaka wangu wa mwisho? Naombeni ushauri wenu!
   
 2. J

  Jamuhuri Huru Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swala lako mimi nalitazama katika pande mbili ambazo ni unaweza kulipwa au usilipwe. Unaweza kulipwa kama ktk makubaliano na mwajiri wako mlikubaliana utaenda kusoma na atakulipa. Hautaweza kulipwa kama hukukubaliana hivyo na mwajiri wako. Katika uzoefu wangu wa siku nyingi wakati nikifanya kazi kwa mwajiri ambaye ni serikali ni kwamba. Mara nyingi serikali ikikupeleka masomoni huwa inakulipa mshahara kama kawaida, sababu yakukulipa ni kwamba tayari mshahara wako ulishawekwa kwenye budget ya mwaka husika kabla hata ujaanza masomo. Kitu nachokiaona hapa ni labda wizi ambao unataka kufanywa na Afisa Utumishi na Mwasibu kwamba mshahara unalipa halafu benk upati.
  Mimi nakushauri swala hili lipeleke kwa wakubwa wako ukiwa umechukua na bank statement zinazoonesha kuwa hakuna pesa iliyoingia wakati pay slip inaonesha ulilipwa. Hii itasaidia kuwawajibisha watu wachache ambao sio waaminifu katika taifa hili changa ambalo linaitaji watu waadilifu ili liweze kuendelea. wako Jamuhuri Huru
   
 3. S

  Sebali Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana bwana Jamuhuri huru kwa ushauri wako!
   
Loading...