Uduvi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2012
- 738
- 518
Ni hatua gani ambayo natakiwa kufuata.Nilimpa pikipiki jamaa mmoja hivi awe anaendesha kwa mkataba wa kuwa ananipa sh elfu 10 kwa siku baada ya miezi Nane pikipiki ingekuwa yake,baada ya wiki tatu tokea nimempa pikipiki akanipigia simu mida ya saa 11 alfajiri kuniambia pikipiki imeibiwa sikukubaliana nae nikamuweka ndani polisi kilwa road kwa siku mbili siku ya tatu akapelekwa mahakamani temeke pale karibu na usalama.Kesi ikendeshwa na mwisho wa siku nikashinda na jamaa akafungwa kifungo cha nnje cha mwaka mmoja na miezi miwili kila siku alikuwa anatakiwa kwenda kuripoti mahakamani na ndani ya iyo miezi miwili alitakiwa anilipe.inshu inakuja kwa mkuu wa iyo mahakama inaonekana amepata mlungula na hafuatilii kujua jamaa kama amelipa au hata kama alilipoti siku aliyopangiwa.nimehangaika sana na jamaa namuona tu mtaani afu mahakama haitendi haki.nilikuwa naomba wabobezi wa sheria mnieleze ni taratibu gani naweza kuzifuata kudai haki yangu,maana nilijbana ili nitusue lkn ndio hivyo navutwa shati nyuma.Msaada tafadhari