Msaada wa kisheria pale inapogundulika huna hatia ya madawa ya kulevya.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,819
26,180
Habari wakuu.

JF ni jungu kuu hivyo halikosi ukoko.

Naona kuna watu wengi wanaenda kuachiwa huru kwa kukosekana ushahidi juu ya shutuma za dawa za kulevya zilizoelekezwa kwao.

Vivyo hivyo Serikali nayo inajipanga namna ya kuwalipa fidia walioshututumiwa bila ushahidi wa kuhusika kwao kwenye shutuma nzito za dawa za kulevya.

Serikali ina pesa nyingi bila shaka za kuwalipa watu fidia. Sasa tujuzane hapa kinaga ubaga namna ya kudai haki kwa waliochafuliwa na kiasi cha fidia wanachoweza kudai.

Ahsanteni
 
Ni ngumu kukukosa wakishakumata hata kwa makosa. Wamekuta msokoto wa bangi na mihadarati kadhaa chumbani kwa Wema Sepetu. Si unajua ukishakuwa teja unasahau hata ulichoitiwa police?:)

Si ajabu wakaikuta pia ofisini kwa Gwajima na kwa Manji. Wonders are always there and shall never end.
 
Wamekaguliwa hawajakuta kitu lakin wanaendelea na mazungumzo
 
Habari wakuu.

JF ni jungu kuu hivyo halikosi ukoko.

Naona kuna watu wengi wanaenda kuachiwa huru kwa kukosekana ushahidi juu ya shutuma za dawa za kulevya zilizoelekezwa kwao.

Vivyo hivyo Serikali nayo inajipanga namna ya kuwalipa fidia walioshututumiwa bila ushahidi wa kuhusika kwao kwenye shutuma nzito za dawa za kulevya.

Serikali ina pesa nyingi bila shaka za kuwalipa watu fidia. Sasa tujuzane hapa kinaga ubaga namna ya kudai haki kwa waliochafuliwa na kiasi cha fidia wanachoweza kudai.

Ahsanteni
Wengine wana husika lakini kwa vile taratibu zilishakiukwa basi tujipange kukabiliana na lawsuits, hamna namna. Hiyo tuhuma ni nzito sana.
 
Ukishinda kesi ya jinai mahakamani wewe shukuru Mungu, hakuna cha fidia hapo. Mambo ya fidia sijui damages ni kwenye kesi za madai (civil cases) na siyo kwenye mambo ya jinai.

Dhana hii ni kutoa wingo mpana wa serikali kum prosecute mtu yo yote inayohisi kafanya kosa la jinai kwani hata ikishindwa mahakamani hakuna hela ya walipa kodi itakayotumika kuwalipa hao walioshinda kesi. Hivyo usitegemee watu kama Lema watakaposhinda kesi, serikali itawalipa fidia kwa kusota mahabusu kwa miezi kadhaa na kuwadhalilisha. Kungekuwa na kipengele cha kuwalipa fidia wanaoshinda kesi za jinai, wajanja wangekitumia kuchota pesa serikalini kwa kusuka deal la kushitakiwa kwa kesi za jinai ambazo wanajua watashinda.
 
Back
Top Bottom