Nilikuwa na kesi mahakama ya mwanzo. Hukumu imetoka haikuwa upande wangu. nina uhakika asilimia zote mdai wangu ametoa rushwa.sasa nimeomba hukumu pamoja na mwenendo wa kesi ili nikate rufaa lakini wananizungusha wiki ya 3 sasa. wiki iliopita karani aliniita na kuniomba rushwa live ili achapishe hukumu. nifanye nini wakuu maana nimebakisha wiki tu ya kukata rufaa. Je naweza kukata rufaa kabla ya hukumu kwa njia ya maandishi haijatoka? je naweza omba hukumu iliondikwa kwa mkono tu na kukata rufaa?