Msaada wa kisheria kukata rufaa

french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
2,875
2,000
Nilikuwa na kesi mahakama ya mwanzo. Hukumu imetoka haikuwa upande wangu. nina uhakika asilimia zote mdai wangu ametoa rushwa.sasa nimeomba hukumu pamoja na mwenendo wa kesi ili nikate rufaa lakini wananizungusha wiki ya 3 sasa. wiki iliopita karani aliniita na kuniomba rushwa live ili achapishe hukumu. nifanye nini wakuu maana nimebakisha wiki tu ya kukata rufaa. Je naweza kukata rufaa kabla ya hukumu kwa njia ya maandishi haijatoka? je naweza omba hukumu iliondikwa kwa mkono tu na kukata rufaa?
 
kamwendo

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
597
1,000
Mkuu, Hukumu lazima ichapwe.

Ile iliyoandikwa na mkono na hakimu inabaki kwenye jalada la kesi husika. Wamekucheleweshea hukumu na muenendo wa case makusudi ili kutengeneza mazingira ya kuomba Rushwa.

Tafuta wakili wa kukusaidia,huwezi kukata rufaa pasipokuwa na hukumu mkononi,na unapokata rufaa kesi yako itasikilizwa mahakama ya wilaya upya,

Ipo hivi nenda mahakama ya wilaya husika mahali ulipo au mahali kesi ilipotoka kusikilizwa mahakama ya mwazo. Ulizia masjala ya wazi utaonana na maafisa wa mahakama waelezee nia yako ya kukata rufaa. Utapewa utaratibu hata kama bado hukumu hujaipata na kuna ada itabidi ulipie. Muhimu kumbuka namba ya kesi husika. Tarehe ya hukumu ilipotoka ni mambo ya kuzingatia,

Usiwaeleze habari za ww kuombwa rushwa na karani wa mahakama ya mwanzo.
Ukitoka mahakama ya wilaya kutegemea na utashi wako unaweza kuamua umshughulikie uyo karani kwa kumripoti PCCB au umuache.

Kamwe usilipie nakala ya hukumu hutolewa bure.
Ningependa kujua upo mkoa gani.
 
french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
2,875
2,000
Mkuu, Hukumu lazima ichapwe.

Ile iliyoandikwa na mkono na hakimu inabaki kwenye jalada la kesi husika. Wamekucheleweshea hukumu na muenendo wa case makusudi ili kutengeneza mazingira ya kuomba Rushwa...
hii hukumu ilioandikwa kwa mkono nilimaanisha wanitolee kopi tu mkuu. haiwezekani niitumie
 
kamwendo

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
597
1,000
hii hukumu ilioandikwa kwa mkono nilimaanisha wanitolee kopi tu mkuu. haiwezekani niitumie
Hukumu haipaswi kutolewa copy inatakiwa ichapwe kisheria na isainiwe.

Miandiko inatofautiana mkuu inaweza kumpa shida uyo hakimu mwengine kuisoma hiyo hukumu utakapoenda kukata rufaa
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
9,377
2,000
Usiombe nakala ya hukumu kwa mdomo, omba kwa maandishi ili hata wakikuchelewesha watakuandikia certificate of delay.
Omba kuonana na hakimu mfawidhi iwapo unahisi unacheleweshwa kwa makusudi.

Kuna ofisi za utumishi sijui kama zipo mahakama ya mwanzo au idara ya utumishi ukifika mahakamani utakuta maelezo na namba zao jaribu kuwasiliana nao wapo makini watakusaidia
 
nimeomba kwa maandishi mkuu, tena siku ile ile hukumu ilipotoka.
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
10,337
2,000
Nilikuwa na kesi mahakama ya mwanzo. Hukumu imetoka haikuwa upande wangu. nina uhakika asilimia zote mdai wangu ametoa rushwa.sasa nimeomba hukumu pamoja na mwenendo wa kesi ili nikate rufaa lakini wananizungusha wiki ya 3 sasa. wiki iliopita karani aliniita na kuniomba rushwa live ili achapishe hukumu. nifanye nini wakuu maana nimebakisha wiki tu ya kukata rufaa. Je naweza kukata rufaa kabla ya hukumu kwa njia ya maandishi haijatoka? je naweza omba hukumu iliondikwa kwa mkono tu na kukata rufaa?
USIOGOPE MKUU HATA WAKIKUPA MWAKANI SIKU 45 ZINAHESABIKA TOKEA UNAPOKEA HUKUMU YAKO SIO SIKU ILIPOSOMWA.

MAKE SURE UNAKABIDHIWA KWA DISPATCH HIYO BARUA
 
french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
2,875
2,000
Kuna idara ya utumishi kila mahakana kuna bango lina namba za takukuru na idara ya utumishi
unazungumzia hili mkuu?
20210329_120128.jpg
 
french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
2,875
2,000
Kesi ilihusu nini na rufaa yako unasimamia kwenye hoja zipi ili tukushauri vizur
kesi ya madai mkuu. nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni flani, tulikubaliana kwa maandishi kuwa nisome masters nikimaliza watanirudishia gharama zote nilizozitumia. Baada ya kumaliza wakanilipa gharama za ada tu niliolipa, ila gharama zingine kama, accomodation, stationery, books, meals, research etc wamekataa kunilipa. wanadai kuwa hizo gharama zingine sipaswi kulipwa sababu nilikuwa napata mshahara, kumbuka mkataba haujasema hivyo
 
SHEDEDE

Member
Feb 6, 2021
55
125

Unazo evidence kwamba ulilipia hivyo? Barua ya admission ilieleza gharama hizo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom